Wapendwa naombeni kujuzwa nahitaji kufanya biashara ya vitenge wp nitapata vitenge kwajumla bila kuchakachuliwa nina mtaji wa mil 1 nataka niwe naviuza kwenye minada, naomba kujua changamoto zaizi biashara.
Vile vipo Kariakoo wanauza kwa Jumla. Changamoto kubwa ni kwenye uuzaji watu wanapokopa kurudisha inakua vigumu hivyo biashara inasuasua. Ila kama ni kwenye minada nadhani siyo ngumu sana kikubwa uwezo wa kupata MZIGO kwa muda muafaka na kuzunguka minadani.
Kama ni vitenge vya kawaida chukua vitenge vya morogoro (ndo jina lake) hata bei yake si kubwa kimoja kwa bei ya jumla ni 5700-5800 kwa kariakoo, kwa minadani utauza sababu vinafahamika kwa wengi na vilijitengenezea jina kwa ubora wake...ila nakushauri ungechanganya na khanga ka wafanya biashara ya kuviuza mnadani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.