Tetesi: Biashara ya vyakula vya mifugo

Tetesi: Biashara ya vyakula vya mifugo

kwe2tu

Senior Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
128
Reaction score
210
Wadau mimi ni rai wa tanzania. Naishi ktk mkoa mmoja miongoni mwa mikoa ya tanzania
Lengo la kuja katika jukwa hili nikutaka kuomba ushauri maana naamini humu kuna wadau wengi wenye dondo ktk maswala ya biashara.
Nina miliki usafiri aina tajwa hapo juu lkn naona km mambo hayaendi kivile nilitaka kuuza hii gari ili niweze kuanzisha biashara ya vyakula vya mifugo mahali nilipo kidogo mzunguko ni mzuri sio haba
Kwahiyo nilitaka kujua km humu kuna mtu mwenye uzoefu wa biashara hii japo nilitaka kuanza na store ya pumba na mashudu
Pumba za mahindi tani 50 na mashudu tani 50.
Maswali yangu
1. Je wazo la kuuza gari ni sahihi
2. Je biashara hii ni nzuri??
3. Zipi changamoto ya biashara hii kwa ambaye anafanya au Alisha wahi kufanya
4. Wapi naweza pata pumba za mahindi, soya na mashudu kwa urahisi na kwabei ndogo ili nipate faida.

Nauomba kuwasilisha
 
Kama wewe ni mkristo au usiye na dini biashara hii ni nzuri sana ukiwa una fuga na nguruwe kibiashara , vile vyakula vinavyobaki au kukaribia kuharibika unalishia na nguruwe utatoka haraka sana.

Nilifanya biashara hii ilinitoa sana kwa mtindo huo.
 
Nina nguruwe na kuku nafuga pia mkuu nipe uzoefu ndugu
 
Kwa kuanzia tu ukitaka kutoka haraka angalau uwe na mtaji hata wa mili 5 mpka 10 ili uweze kuwa na aina zote za vyakula na virutubisho mbalimbali pamoja ma mizani.

Hakikisha unapanga frem kubwa yenye nafasi kubwa kwa njee kwa ajili ya kuchanganyia vyakula na store za kutosha kwa kuhifadhia mzigo wako.

Pata elimu ya ulishaji mifugo, namna ya kuchanganya mchanganyiko mzuri , ambao utafanya mifugo itoke kwa haraka , hii itakua ni silaha bora kabisa ya kuwaangusha wapinzani wako , kwa sababu wateja huzingatia hilo, mafunzo unaweza yapata youtu.be au kwa wataalamu.

Biashara hii itakuhitaji wewe na msaidizi mmoja au wawili.

Ukiweza kujenga mahusiano mazuri na boda boda , watakuungisha sana pale wanapoagizwa mzigo .

Kama gari yako ni yakutembelea uza , kama ni ya kazi mfano kirikuu unaweza tafuta mtaji kwa njia nyingine , hiyo gari itakusadia kuwapelekea wateja wako mzigo .

Hii biashara ukipata eneo zuri la wafugaji unatoka fasta mno kukunja 200k kwa siku sio jambo la kuuliza.

Ukiweka na ufugaji wako wa nguruwe utawalisha kwa hiyo biashara , wakikua Chinja mwenyewe uza kwa kilo .
 
Nashukuru sana mkuu kwa nondo zako umenisaidia sana kwa mawazo. Gari yangu ni raum new model
 
Mambo sio rahisi namna hiyo mzee
 
Wadau mimi ni rai wa tanzania. Naishi ktk mkoa mmoja miongoni mwa mikoa ya tanzania

4. Wapi naweza pata pumba za mahindi, soya na mashudu kwa urahisi na kwabei ndogo ili nipate faida.

Nauomba kuwasilisha
Mkuu hutaki watu wajue uko mkoa gani halafu unauliza utapata wapi raw materials? At least sema hata kanda uliyopo, kama mkoa ni wa siri sana. If at all you need detailed information about the business.
 
Sijaficha bosi nipo mwanza jiji
Mkuu hutaki watu wajue uko mkoa gani halafu unauliza utapata wapi raw materials? At least sema hata kanda uliyopo, kama mkoa ni wa siri sana. If at all you need detailed information about the business.
 
Nipo mwanza jiji
Safi sana huko raw materials za kutosha, na ukishaanza mdogo mdogo nenda kafanye research kenya, kule ukiuza chakula cha mifugo wewe ni tajiri. Na hata kwa mtaji mdogo kuna watu wanachukua dagaa reject na kupeleka huko kama raw materials ya chakula cha kuku. Wanapiga hela sana. Nenda mwaloni kafanye research utawakuta wengi tu wanaofanya hizo kazi, unatoa kama 10,000 kwa wale vibarua wanakupa mchongo mzima.
Kwa mashudu kama ya pamba yanapatikana sana viwandani kipindi cha msimu. Viwanda vingi vipo bariadi na kwingineko. Cha muhimu tembea tembea hayo maeneo kafanye research kabla ya kuanza, pumba zinapatikana mashineni zile kubwa kubwa zinazo process unga wa packaging, unawatangulizia pesa wanakukusanyia. Kikubwa jenga tu mahusiano na watu. Information nyingi utaipata ukiwa ground, zaidi uwe unatoa kuanzia 5,000 mpaka 10,000 kwa mtu unayeona anaweza kuwa na data, hii njia naitumiaga sana kukusanya data na inawork.
 
Asante mkuu umenifungua sana
 
Back
Top Bottom