Biashara ya zabibu kati ya dodoma na nairobi.

Biashara ya zabibu kati ya dodoma na nairobi.

Ba Martha

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2010
Posts
349
Reaction score
107
Ndugu wanaforum!
Salam,

Ninaishi Arusha...Nimepata mtaji ( 5 m).. katika kuwaza biashara ya kufanya ili nami nitoke kimaisha nimeona nijaribu hii ya kuchukua zabibu kutoka Dodoma na kuziuza Nairobi..ingawa ni ya msimu lakini naamini ni good start..Ningependa kujua a,b,c ya hii biashara kwa wale ambao mko familiar nayo hasa katika nyanja za masoko, usafiri, usumbufu wa boda, kodi n.k ..Naamini ntapata ushauri wa kutosha kutoka kwenu.

Mungu awabariki.
 
Wataalam wa hii biashara njooni mumjibu mdau ili nasi tupate mwangaza wa hii biashara.
 
mkuu agrobuz..wadau naona bado wanandaa nondo..tuvute subira.
 
Hilo ni wazo zuri. Tunahitaji kuuza zaidi nje kuliko kununua.
 
Ni kweli kabisa tunahitaji kuuza nje, ila siyo tusifikirie kwenye produces only tuweke mtazamo kwenye byproducts za hizi produce. Nahisi kwa hapo utatoka zaidi na kuna niche markets nyingi unaweza kujipenyeza na ukakuwa kiuchumi ndugu zangu. Ni mtazamo tu
 
Kuna mdau mmoja ndio ishu zake...kaahidi kunipa info kati ya leo au alhmisi atakapopita hapa a twn..nami ntatoa feedback hapa jf..sababu naona wadau wengi hawana ujuzi na hii biashara.
 
Kwanza anza na kibali kinaitwa Plant Import Permit kinatolewa kule mzigo unapoenda Omba kitengo chao Kenya kinaitwa KEPHIS
Bila ya kibali hicho utasumbuliwa sana boda na wanaweza wasikukubalie kabisa
Ukishapata nenda boda ya tanzania pamoja na issue za customs utahitaji cheti cha usafi kinaitwa Phytosanitary certificate ambacho kitaambatana na hiyo plant import permit uliyoomba kabla
Kumbuka import permit inatakiwa kuombwa kabla hujaandaa mzigo
Kama una maswali ni PM tutaongea kwenye simu
 
Thanks mkuu Denis..ntakupm kwa ufafanuzi zaidi..
 
Usijali Agribuz..kila kitu kitaanikwa jamvini..
 
Back
Top Bottom