Enkulu
Member
- Sep 29, 2022
- 20
- 76
Leo nimekaa nikaanza kutafakari hili, nikajiuliza mtu anafungua kiwanda cha kutengeneza viberiti, analipa wafanyakazi, analipa kodi ya serikali pamoja na vitu vyengine, ananunua materials, analipia usafirishaji alafu kiberiti anakuja kutuuzia kimoja 100/=
Nachoamini ukiona mtu anafanya biashara fulani ujue inampa faida japo hasara hutokea lakini faida hupatikana mara kwa mara.
Ina maana ya kwamba kwenye hio 100/= huyu mtu faida yake ipo humo humo. Sijui ni shillingi ngapi lakini ipo.
Mtaani kuna wamama wengi wanachoma maandazi, hivi ni kuchoma au kukaanga? Hivyo hivyo bana turudi kwenye mada. Wamama hawa sio kwamba ni masikini lakini hali zao ni za kawaida, wengine kawaida mno.
Lakini mbona Bakhresa nae akaja kuuza hayo hayo maandazi? Tena kwa bei hio hio kama wao. Unajua kwanini? Bakhresa hauzi mtaani, soko lake kalipanua vibaya mno. Yeye anauza maandazi nchi nzima.
USHAURI WANGU; Nadhani fikra zetu zianze kuangalia hili, tuanze kuzingatia hizi biashara zinazoonekana zina faida ndogo alafu tafuta namna ya kupata hio hio faida ndogo ila ije kwa wingi.