Biashara za kuuza bidhaa mitandaoni:Watanzania wengi hawana uelewa juu ya hilo

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Katika mambo ya kushangaza ni kuwa kuuza biashara kupitia mitandaoni kama facebook,insta,jf Na kupatana nimenote kuwa Watanzania wengi hawajui kufanya biashara.

Jee ni kivipi hawajui?
Unakuta bidhaa ya 5000 dukani yeye atauza 20000 sasa hapo utapata wateja kweli???

Mboga za majani za 500 yeye atauza 3000
Nazi ya 500 yeye atauza 1200

Sasa hapo unaona ni bora ununuwe dukani tu
Mchele kilo wa 2000 yeye atauza 4000 hapo hujaweka delivery

Tujifunze kwa wenzetu ambao huuza bei sawa na madukani au bei iliyopo hii inawafanya hata watu washawishike kununua bidhaa zako mtandaoni...kuliko kuuza ghali bidhaa zikudodee
 
Tatizo wanauza mitandaoni sasa wengi ni madalali kuliko wenye maduka au bidhaa bei wanayoiongeza ni mara mbili ya bei dukani.

Huu mtindo upo jumia sana baada ya kuruhusu watu waanze kuuza bidhaa.
 
Umesema sawa.Ndo maana wenzetu wanaendelea kama Alibaba.
 
Tatizo wanauza mitandaoni sasa wengi ni madalali kuliko wenye maduka au bidhaa bei wanayoiongeza ni mara mbili ya bei dukani.

Huu mtindo upo jumia sana baada ya kuruhusu watu waanze kuuza bidhaa.
Cha ajabu wanaofanya huo mchezo wanawafanyia watu ambao wako Dar pia. Kwa nauli isiozidi 2000 utafika kariakoo na kurudi kwako ukiwa na bidhaa ile ile kwa bei ya chini kuliko bei ya kwenye kurasa ya instagram.
 
Unaofanywa na ma winga! Kitu cha elfu 50,000 wao watakuandikia 70,000! Cha 60,000 unaandikiwa 85,000! Ukienda kariakoo ukavikuta na bei zake halisi utacheka.

Increment ni 15-20k toka kwenye bei halisi.
 
Uchawi upo, tumeamua 'kujiajiri' kama mlivyotushauri..... bado mnataka tufanyeje sasa..?
 
Pia uaminifu hakuna.
 
Uchawi upo, tumeamua 'kujiajiri' kama mlivyotushauri..... bado mnataka tufanyeje sasa..?
Uzuri mdomo haulipiwi kodi, kama ingeanzishwa kodi ya mdomo nadhani bongo tungeongoza kulipa kodi mkuu. Tuvumilieni tu
 
Dasilama watu wanayo hela ila hawana muda, vijana wanaishi kwa njia hizo halali bila kodi za fremu wala mitaji mikubwa..... we ukifika bei anakimbia Kariakoo anakuletea na utasikia 'free delivery' sasa we unateseka nini..?
 
Viatu vyote insta vinauzwa 150k sijui wameambiana bei..wakati ukienda kariakoo unapata kwa 80k
 
Viatu vyote insta vinauzwa 150k sijui wameambiana bei..wakati ukienda kariakoo unapata kwa 80k
Shati 25,000 wakati kariakoo 15000,bado umpe na gharama za kuleta mzigo,unakuta ni gharama tupu bora ukazunguke tu mwenyewe
 
Ila si vyema kupandisha bei kiasi kwamba watu wanastuka labda iwe 150k bei halisi alafu unauza 160k nafikiri ingefaa
 
Mimi nilikuta tangazo instagram la Printa inauzwa kwa 360,000/=,
Nilipofika Kariakoo karibu na dukani kwao nikawapigia simu wakaniambia ni 435,000/= imejumuishwa na gharama ya VAT.

Nikageuka zangu,
Nikaenda kununua maduka ya Wasomali,
Nikasepa.
 
Ila mbona nasikia alibaba nao kuna utapeli kuna ukweli hapo?
Hao sio Alibaba bali ni Ma-alibaba yaani watu feki wanaojifanya Alibaba.Ndio maana ukiona akaunti ya kampuni inayofanya vizuri sokoni kuna watu wengine wengi hufungua kama hiyo au inayofanana na hiyo ili wawapige watu hela.
 
Mimi nilikuta tangazo instagram la Printa inauzwa kwa 360,000/=,
Nilipofika Kariakoo karibu na dukani kwao nikawapigia simu wakaniambia ni 435,000/= imejumuishwa na gharama ya VAT.

Nikageuka zangu,
Nikaenda kununua maduka ya Wasomali,
Nikasepa.
Hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…