SoC03 Biashara za Wafanyakazi wa Umma zinaleta Migongano ya Kimasilahi na Upendeleo

SoC03 Biashara za Wafanyakazi wa Umma zinaleta Migongano ya Kimasilahi na Upendeleo

Stories of Change - 2023 Competition

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
BIASHARA ZA WAFANYA KAZI WA KAZINI ZINA PELEKEA UPENDELEO NA MIGONGANO YA KIMASILAHI

Kufanya biashara ukiwa offisini sio jambo baya kabisa ni sehemu ya kujiongezea kipato, kwa sababu ni vigumu sana kuishi kwa kutegemea mshahara wa mwezi, hivyo njia pekee ni ya kufanya kazi za kando wanaita nah ii ipo Dunia nzima.

Tatizo lilipo ni aina ya Biashara inayo fanywa na huyu mtumishi wa umma, hapo ndio sehemu ambapo lazima mamlaka zikae chini kuangalia kama ni sawa au la, nitatoa mifano ya migongano mikubwa ya kimasilahi, na ushindani usio huru inayo fanywa na watumishi wa umma wanao fanya biashara sawa na zile idara wanao simamia.

Askari wa Barabarani kumiliki Daladala; Hii kwangu ni kosa kubwa ambalo halipaswi kufumbiwa macho na sio tu ni mgongano wa kimasilahi bali pia ni kinyume na fair competitions, sio rahisi ukamate Daladala ya askari, hawa wanapigiana simu tu kazi zinaendelea, na wanao hangaishwa ni raia wa kawaida wenye biashara ya Daladala. Hii ni jambo linapaswa kuangaliwa na na taasisi zinazo shughurikia mambo ya utawala bora na pia hata Tume ya Ushindani huru wa kibiashara Tanzania kama jambo hii ni sawa.

Wafanya kazi wa Mamlaka ya Mapato kuwa na Biashara. Hili ndio eneo ambalo kama nchi inataka kupambana na rushwa inapaswa kuliwekea mkazo, ni nani ataenda kufunga biashara ya mfanyakazi wa TRA? Je wanalipa Kodi stahiki? Nani anakagua kujua kwamba hawa wamelipa kodi inayo takiwa kulipwa? Je TRA wana kitengo cha kuangalia wafanya kazi wake wenye biashara? Hakuwezi kukwa na ushindani huru kama kwenye biashara mnashindana na watumishi wa Mamlaka za mapato ambao na wao wana biashara kama inayo fanywa na raia wengine wa kawaida.

Wafanyakazi Jiji/Manisapaa/Halimashauri Idara ya Biashara na wao kuwa na Biashara; Hii sio sawa hawa wanapaswa kuwa walezi wa biashara zote lakini pale na wao wanapo kuwa wako ndani ya uwanja wanacheza mpira ilihali wao ndio waamuzi kunaondoa ushindani huru wa kibiashara pia, na hii inaanza kuzaa kupendeleana kwa kila njia.

Dakitari/Mganga mkuu wa Hospitali ya Umma kumiliki Hospitali au Duka la Dawa; Hii inawezekana Tanzania pekee, na ni wazi kabisa kuna mgongano mkubwa sana wa kimasilahi hapa, ni kawaida Hospitali ya umma Dakitari anakupa appointment mkutane hata weekend kwenye Hospitali yake au Duka la dawa, nashindwa kuelewa kama mamlaka hazioni kwamba hili ni tatizo kubwa sana, linazaa upendeleo wa wazi kabisa, wizi na Mganga mkuu wa Wilaya anapo kuwa na Hospitali yake binafisi lazima ajipendelee kwa kila namna na kuna wakati hata vifaa vya umma atavitumia kwenye kazi zake binafisi, hapa kuna kuwa ile fair competition haipo kabisa.

Afisa elimu wa wilaya anamiliki Stationary; Unategemea kuwe na ushindani huru kama afisa mkuu wa elimu na yeye ana Duka la vitabu na vifaa vingine vya shule? Hapa hata wakuu wa shule watakuwa wanaend a kununua vitu Dukani kwake ili kutafuta kupendwa au kwa kuhofia wanaweza fanyiziwa,haya ni mambo ambayo sielewi kwa nini watawala wanayona na kuyafumbia macho kabisa.

Afisa Kilimo ana Duka la pembejeo za kilimo na mifugo; Hii inazaa upendeleo wa wazi kabisa, na hakuwezi kuwa na ushindani huru hapa zaidi ya kujipendelea kwa kila namna, vitu kama hivi havipasiw kufumbiwa macho.

Mawaziri wa wizara kuwa na Biashara inayo endana na wizara yake; Kuna wakati kulikuwa na naibu mmoja wa wizara ya Afya alikuwa na Chuo cha afya, hii hata mtoto mdogo anaweza kukuambia sio sawa kabisa, unakuta waziri wa Mali asili na utalii ana kampuni ya Utalii, hili lisha toke asana, na unakuta linapigiwa kelele lakini hakuna anaye jail.

Kuna Idara nyingi taasisi nyingi zenye haya matatizo nimetaja chache tu kwa mfano ila zipo kuna mashirika ya umma huko, unakuta Mfanya kazi wa Shirika la kusambaza maji ana biashara ya kuuza maji kwa kutumia maji wanayo sambaza. Mifano ipo mingi na wadau mtasaidia kutaja mifano mongine.

Haya yametokea sana na yameisha lalamikiwa sana, na mifano ipo sana, unakuta Dakitari anakamatwa na vifaa vya Serikali kwenye Hospitali binafisi, ilisha tokea snsa wenye daladala kulalamika kwamba Daladala Fulani na Fulani huwa haziguswi kwa saabu ni za askari fulani.Haya yanavunja sana moyo kwa wafanya biashara wengine ambao wao hawana nafasi hizo na Serikali inapswa sana hili kuja kuliangalia halipaswi kuendelea.

Kwa wanao fanya kazi Mashirika binafisi hasa hizi NGOs za Kimataifa watakubaliana na mimi jinsi walivyo na sheria kari sana zinazo husiana na migongano ya kimasilahi, ambapo mfanya kai lazima atangaze kama ana mgongano wa kimasilahi na asipo fanya hivyo ikaja kugundulika baadae inakuwa ni kosa kubwa sana la kumfukuzisha kazi. Waliona mbali ingawa pia ni mambo yanafanywa na nchi zao huko waliko tokea. Ila kwa Tanzania hili jambo tunalichukulia kawaida sana.

Nini nashauri kwa mambo kama haya, ili basi kuwepo na ushindani huru na kuondoa upendeleao ulio jificha na pia migongano mikubwa ya kimasilahi;

Watumishi wa umma asifanye biashara inayo endana na sekita au Idara anayo isimami, kama hawezi achague moja biashara au kazi, ni lazima mtumishi atumike watu wote sawa, mtumishi kama anataka kufanya biashara ya kazi anayo ifanya basi angoje kustafu au atangaze wazi na kuwe na mamlaka za siri za kuangalia mwenendo wa biashara yake kuhakikisha hakuna aina yoyote ya upendeleo.

Kuwaondoa kwenye Idara za kufanya maamuzi linapo kuja swala linalo endana na biashara anayo fanya, Mfano Mganga mkuu wa Wilaya ana Hospitali na kuna kikazo cha Kujadili jinsi ya kudhibiti Hosipita binafis au jinsi ya kuziinua Hospitali binafisi, hapo unategeme nini? Hivyo basi Mganga mkuu wa wilaya asiwemo kwenye vikao vya ina hio kabisa.

Nawasilisha kwa mjadala wa jinsi gani tunaweza omdoa hili, na sio swala la kuonenea wivu bali hili ni tatizo kubwa sana, kuna watu wanaweza ongea mambo ya wivu na kadhalika ila kama usha fanya biashara na ukawa unashindana na nilio taja hapo juu utakubaliana na mimi kwamba hili ni tatizo kubwa sana Tanzania.
 
Upvote 3
Nisaidie kurekebisha Kuchwa Cha habari.

BIASHARA ZA WAFANYAKAZI WA UMMA ZINALETA MIGONGANO YA KIMASILAHI NA UPENDELEO
 
Habari Mkuu,

Aisee, hongera kwa andiko lako makini lenye tija kwenye jamii.


Kura yangu umepata.

Naomba kura yako kwenye andiko langu linaloonyesha mikakati ya kufanya kutatua changamoto zilizoorodheshwa kwenye ripoti ya CAG. SoC03 - Tujibu Ripoti ya C.A.G
 
Back
Top Bottom