Tayari una soko ?, nadhani hapo ndio pa kuanzia ukishapata soko la kupeleka mayai kinachobaki ni kutafuta reliable source (sehemu tofauti tofauti) sio kwa mtu mmoja ili anayekuuzia mmoja akikosa uchukue kwa mwingine.., baada ya hapo ni kubargain na kununua kwa rahisi kadri inavyowezekana ili unapouza uongeze profit margin.
Pia usisahau kuweka gharama ya kuyasafirisha unapoyatoa na risk iwapo baadhi yakiaharibika au kupasuka bado faida yako isitetereke. Pia hata yakipasuka kidogo unaweza kujaribu soko kwa wauza chips mayai kuwauzia kwa bei nafuu