Bibi Titi Memorial Festival Ikwiriri Rufiji: Bibi Titi Katika Vikao Vya Ndani Vya MIkakati Kupanga Mikutano ya Mwanzo ya TANU Mnazi Mmoja na Jangwani

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Aisha "Daisy" Sykes mtoto wa kwanza wa Abdul Sykes anasema akiwa msichana mdogo alishuhudia pirikapirika zote nyumbani kwao akimuona Bibi Titi, Bi Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee na akina mama wengine wakishiriki katika vikao vya ndani nyumbani kwao Mtaa wa Stanley na Sikukuu kupanga nini akina mama wafanye katika mkutano wa TANU kesho Mnazi Mmoja.

Hivi vilikuwa vikao vya kutaka kwanza kuwajaza watu uwanjani na pili kuupamba mkutano upendeze na kuitia nguvu TANU.

"Nimesikia mazungumzo mengi wakati baba na wenzake akina Mwalimu Nyerere, Mzee Rupia na Dossa Aziz walipokuwa wakijadili majina na shughuli ambazo hawa akina mama walikuwa wahusishwe ili kuleta mvuto wa kisiasa katika mikutano yao ya TANU.

Nakumbuka vizuri sana jinsi baba alivyokuwa karibu sana na Mwalimu Sakina na ndugu yake Mwalimu Fatna Watoto wa Bi Chiku bint Said Kisusa."

Akina mama hawa wote walimtazama Bibi Titi kama kiongozi wao.


Bi. Tatu bint Mzee

Aisha ''Daisy'' Sykes


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…