zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Habari za jioni wana JF, ni muda mrefu kidogo sijaweka mada humu ila leo tupate wasaa kidogo tukumbushane mambo machache kuhusu Bible.
NB: Angalizo hii mada ni purely objective tusiiweke kidini na kuanza kashfa, matusi na kejeli kwa imani fulani. Natamani iwe hoja juu ya hoja ili wote tujifunze.
Utangulizi
Kumekua na contradiction sana kwenye vitabu vya gospel hata kwa vitu vidogo tu mfano tarehe ya Yesu kuzaliwa na kufa ama Story ya wale wafungwa pembeni ya Yesu msalabani n.k. Na huu mkinzano unawapa fursa watu kuiona Biblia kama nadharia tu au hadithi za kufikirika (Myhtology) na sababu kuu ni taarifa kadhaa kukinzana.
Kutokuwepo kwa vyanzo halisi vya injili nayo imekua changamoto na inafikia wakati watu wanahoji uhalisia wa matukio ya kipindi cha Yesu. Yaani yalikua verified wapi ama version ipi ya vitabu vya injili ni credible zaidi. Ili kusolve haya yote wanatheolojia walijaribu kujikita katika kutafuta vyanzo vya vitabu vya injili.
Q Source
Msimamo uliopo kwenye ulimwengu wa kitheolojia na imani ni kwamba kitabu cha kwanza kuandikwa ni Marko maana ushahidi ni kwamba Mathayo na Luka wamenakiri masuala mengi kutoka injili ya Marko. LAKINI kuna maandiko yaliyopo katika Mathayo na Luka ILA hayapo kwenye injili ya Marko. Hiko chanzo cha pili kikapewa nickname ya Q yaani Quelle source.
Chanzo hiki kina nadharia mbili kwanza; ni simulizi za moja kwa moja walizosikia hao waandishi wa Mathayo na Luka kutoka kwa Yesu na wanafunzi wake. Nadharia ya Pili ni kwamba ni maandiko yaliyoandikwa yakiwa na yamenakiriwa original kabisa kutoka kwa Yesu ama wanafunzi wake.
Kupitia nadharia ya pili swali linakuja.... Je Q source iliandikwa na nani?
Q source kwanini isingekua kitabu kabisa kwenye Biblia?
Je kilifichwa ili kuondoa ukweli wa taarifa fulani?
Kuondoa Sintofahamu
Ikumbukwe kma Q source ni original script yenye uhalisia zaidi. Ingesaidia kuondoa sintofahamu hasa kwa kukinzana kwenye masuala kadhaa ya kibiblia mfano nitoe
Mathayo 2:1 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Herode (4 BC) ila Luka 2:2-3 inaonyesha Yesu alizaliwa kipindi cha Governor Quirinius (6 AD). Ila kungetumika source moja tu mfano hyo Q source ingesaidia kuondoa discrepancy zote zilizopo na kuweka msimamo mmoja wa Injili.
Mat 12:39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona
Marko 8:12
12 Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.
Mfano hapa je mtu wa kizazi kile ataamini kipi? Yesu alitoa ishara ama hakutoa yoyote? Je haiwezi mchanganya mtu kiimani?
Hitimisho
Nimeleta mada ili tujadili hapa je Q source ipo? Na kama Ipo Iko wapi? Je ingeweza kusaidia kuondoa ukinzano? Je ukinzano huu wa injili hauondoi credibility ya Biblia kma kitabu kitakatifu (maana tunaamini imeandikwa kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu)
Karibuni kwa mjadala