Biblia kwa Jicho Jingine

wafuasi wa rangi za upinde wa mvua mmeshatuharibia uzi
 
Naomba kwa mwenye kujua jinsi ya kupata post hii "Biblia kwa jicho jingine" umeandikwa na jamaa anayejiita Bilionea ......anisaidie tafadhali
 
Asante sana ndugu umezidi kunidhibitishia kauli ya kiongozi mmoja wa dini aliwahi kuniambia kwamba hakuna jehanamu wala hakuna pepo au mbingu kama tunavyo aminishwa.
Kwamba kuna mahali ambapo ni motoni au mbingu ni hakuna.

Kama ulivyo sema kwamba roho inapambana kurudi kwenye asili yake, adhabu kubwa kabisa ambayo itapata roho iliyokua ovu ni kutokumuona Mungu milele.
Kwa asili ya roho kutokuonana na Mungu ni adhabu kubwa sana , na hilo ndio litakalowapata watu wote na vyote vilivyo viovu na si kuchomwa moto kama inavyo semekana.

Na huo pepo au mbingu sio sehemu ya kuimba na kusifu wala sehemu ya kula raha na starehe za kibinadamu bali ni ile hali ya roho kukutana na Mungu.

Hivyo vya kupewa pepo ya daraja la kwanza au la mwisho au kuchomwa moto ni imagenetion ya kibinadamu tu.
 
zote hizi ni nadharia tu
 
Kiranga nawe matope TU kichwani. Yaani Kwa mawazo Yako unafikiri unaweza mpangia Mungu namna ya kuendesha mambo ?

Nani alikuambia nikiwa na uwezo wa kujua utatenda Nini ndio iwe sababu ya kutokukuazibu ukitenda ? Mbona ujiulizi wewe unayetenda huo uovu wewe ujui kama ulitendalo ni uovu na una uamzi wa kutenda au kutokutenda. Hoja yako ni mfu coz unataka kuondoa uwajibikaji na utashi wa mwanadamu kwa lile alifanyalo. Shupaza shingo Yako na ukifa bila kutubu Chamoto utakiona .

Nani alikuambia coz nina upendo wote why nawachukua wapendwa wako ? This rediculous and pathetic ...toka lini una question upendo wa Mungu kwa kuondoa wapendwa wako. Nani ajuae wafu wanapokwenda wanapofariki? Unazani wana raha sana kuishi Dunia ya watu wabishi na jeuri kama wewe ! Nani ajuae hao wanaoachwa ndo Mungu anawapa fursa ya kulelelewa na watu watakaowasaidia zaidi? Process ya kutambua upendo wa Mungu sio lazima ueleweke kwenye fahamu zako. Njia za Mungu zipo juu ya jinsi unavyotafsiri wewe.

Contradiction ya kiuandishi sio quarantee ya contradiction of the reality. Ni kweli dini ni nyigi na Kuna details zinapishana ila mantic inabaki kuwa ileile . Dini zote zinajaribu kujibu chanzo Cha maisha ya hapa duniani ni kipi, mwanadamu ni nani, Nini kusudio la maisha yake, hatima ya mtu akifa ni nini etc, kufafanua maswali hayo Kuna dhana nyingi zinafafanuliwa ila life dynamics and it's manifestations it tells all...

Mungu ni wa kuaminiwa

Mungu ni wa kutumainiwa

Ukimwamini poa usipomwamini yeye anabaki kuwa wa kuaminiwa
 
Hata kama mimi ni matope tu kichwani, hilo linaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba viumbe kama mimi walio matope tu kichwani.

Pia, huelewi tofauti ya logical consistency na kumpangia Mungu.

Ukisema wewe una urefu wa futi sita, nikataka tuhakiki kama kweli una futi sita, hapo sijakupangia uwe na futi sita, nahakiki kama dai lako lina ukweli. Nikiona hujafika futi sita na kusema wewe una urefu wa futi tano, ukinijibu nisikupangie uwe na futi sita, utakuwa huelewi kwamba mimi sijakupangia uwe na futi sita, nmehakiki maneno yako tu.

Zaidi, mimi siwezi kumpangia kitu Mungu, hilo ni kweli. Kwa sababu Mungu hayupo.

Nitampangiaje kitu Mungu ambaye hayupo?

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Mathayo 11:5
''vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.''

Hatuwezi kuamini kwa kulazimishana ikiwa wewe umehubiriwa juu ya habari njema na wewe ukakataa nitakuwa Mjinga sana kama nikaendelea kukulazimisha,nitaacha Mungu ashughulike na wewe.

Tusisumbuane eti tuthibitishe uwepo wa Mungu kisayansi wakati kila siku tunaona matendo Yake.
 
Unaji contradict.

Unanihubiria, halafu hapo hapo unasisitiza hatuwezi kulazimishana.

Mimi sitaki kuhubiriwa, tukianza mahubiri naweza kukushinda wewe kwa mahubiri.

Mimi nataka facts, proofs. Unaweza ku prove Mungu yupo?
 
Unaji contradict.

Unanihubiria, halafu hapo hapo unasisitiza hatuwezi kulazimishana.

Mimi sitaki kuhubiriwa, tukianza mahubiri naweza kukushinda wewe kwa mahubiri.

Mimi nataka facts, proofs. Unaweza ku prove Mungu yupo?
Hata kama utaweza kunizidi kuhubiri kwangu itakuwa furaha zaidi maana sisi hatufanyi hivyo kwa kutafuta utukufu wetu bali ni Kwa Utukufu wa Mungu.
 
Proof nyingne unayotaka ya nini na ikisaidie nini wakati una msimamo wako.Ishi maisha yako, na kama unataka proof msubiri atakuja kukupa yeye mwenyewe
 
Hata kama utaweza kunizidi kuhubiri kwangu itakuwa furaha zaidi maana sisi hatufanyi hivyo kwa kutafuta utukufu wetu bali ni Kwa Utukufu wa Mungu.
Huyo Mungu hayupo.

Habari ya kuwapo kwake ni hadithi tu ilitungwa na watu.

Ukibisha, thibitisha yupo.
 
Proof nyingne unayotaka ya nini na ikisaidie nini wakati una msimamo wako.Ishi maisha yako, na kama unataka proof msubiri atakuja kukupa yeye mwenyewe
Wewe unahubiri hapa. Unahubiri kitu ambacho huwezi kukithibitisha?

Unahubiri uongo siyo?
 
Labda ungeonyesha kwanza chanzo cha habari ya makala yako - mfano wapi imeandikwa Mungu akisema yeye ni "Mungu Baba" etc. Lengo la uandishi ni kutoa habari inayosimama yenyewe, lakini makala yako haya yana habari za kupika na hayatokani na utafiti ulioufanya kwa sababu kama ingekuwa hivyo angalau ungeonyesha marejeo ya vyanzo vyako au hata utafiti wa watu wengine wenye 'conclusion' kama ya kwako. Katika yote haya jambo muhimu likiwa 'intellectual humility'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…