Biblia kwa Jicho Jingine

Ni kweli kabisa mkuu.
Ndio maana stori hii inasadifu kichwa chake cha habari, kwamba ni masimulizi ya Biblia kwa jicho jingine.

Nakubaliana na wewe kuwa dini nyingine nazo zina versions zao, lakini kujifunza mambo ya wengine ni jambo jema pia ili kupanua ufahamu na kuelewa yale ambayo ulikuwa huyajui.

Mimi Quran naisoma pia mkuu, lakini sijapata wasaa wa kuichambua kwa upana, ila nikipata nitaichambua pia.
Ila kama kuna mtu pia anafahamu historia ya dunia kwa jicho la Quran au dini yoyote au kitabu chochote anaweza kuileta hapa, ila cha msingi tu mjadala usianze kuwa wa kidini na kuaza sarakasi za kidini tulizozoea humu JF....
 
...nimekuelewa saaaana mkuu...umejibu vizuri na vema kabisa
...let's go
 
Mkuu nilichokielewa pia nikumegee kidogo .Mimi kama Mimi nimegundua pia uelewa Wa kila binadamu mmoja pia ndio uelewa wake wakumjua Mungu. na hiyo ni sana Kwa sbb Mungu anajifunua Kwa yeyote na Kwa njia mbali mbali. Mungu hana umbo halisi wala tabia iliyo moja .na kila mmoja anampa ufahamu kadri atakavyo yeye.
 
Mimi ninavyojua kutokana na Biblia, Mungu ni mmoja, ila amefanya kazi kuu tatu ambazo amezitambulisha kwa sisi binadamu.
Kazi nyingine alizozifanya hazijatambulishwa kwetu na hatuzijui.

1. UUMBAJI
Hii ni kazi ya kwanza ya Mungu kuitambulisha kwa binadamu, kitabu cha Mwanzo kinaeleza jambo hili vizuri.
Kazi hii ndiyo inayompa Mumgu cheo cha Muumbaji, au Baba.
Baba ndiye mzalishaji, ukisoma kitabu cha Mathayo 1 - 1..utaona jinsi baba alivyo na nguvu ya uzazi.
Hivyo majina ya Muumbaji, Baba yanalenga kuienzi kazi ya Mungu ya Uumbaji.

2.UKOMBOZI
Baada ya kuumba ulimwengu na vyote viujazavyo Mungu aliipenda kazi yake. Kukatokea tatizo la huyu kiumbe binadamu, kwakuwa Mungu alimpa binadamu akili, hekima na uhuru wa kuchagua jema na baya.
Binadamu akakengeuka na kumuasi Mungu na kupoteza mahusiano yake mema na Mungu wake.
Mungu aliupenda sana ulimwengu akaamua kuja mwenyewe kwa umbo la binadamu ili awape binadamu kweli yake wakati akiishi nao pamoja.
Ndipo alishuka na kuvaa umbo la binadamu Yesu Kristo.
Ili watu wamwamini na kumsikiliza akaamua kujitambulisha kwetu kama Neno au Mwana wa Mungu.
Yohana 1 : 1....
Maana angejitambulisha kuwa,
" mimi ndiye Mungu "
watu wasingemsikiliza hata kidogo. Ila kazi alizozifanya zilimtambulisha kuwa yeye ni Mungu kamili.
Mfano kazi aliyoifanya ya kumuumba upya Lazaro aliyekufa.
Akafundisha kweli yote ya Mungu na kurudi kwake Mbinguni.
Hivyo basi, Mungu aliikamilisha kazi ya ukombozi kwa kutumia Jina la Yesu Kristo. Ndio maana Yasu alipofufuka alisema.

" nimepewa mamlaka ya Mbinguni na duniani"

Hivi mwenye mamlaka ya mbingu na duniani nani ?
= Mungu pekee.

Hivyo Mungu huyohuyo mmoja alikamilisha kazi ya kuukomboa ulimwengu kwa kutumia jina la Yesu Kristo.
Na akatuagiza tuombe chochote kwa jina la Yesu na sio jina jingine lolote.
Jina Lipitayo Majina Yote ni Mungu.

Isaya 9 : 6. Inasema

"Maana kwa ajiri yetu mtoto amezaliwa.
Tumepewa mtoto mwanaume,
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake.
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele
Mfalme wa amani "

Ona hapo Isaya anamwita Yesu majina yote mawili
Mungu Baba, muumbaji
Mungu Mwokozi, wa ulimwengu

3. UWEPO WA MUNGU.
Tukijikumbusha kitabu cha Mwanzo kuna mahali pameandikwa, Roho wa Mungu akatulia juu ya maji.
Tukirudi kwa Agano jipya Mungu, Yesu anasema anamleta msaidizi ili aendelee kuishi nasisi muda wote akitulinda na kutukumbusha maagizo ya Mungu.
Huyu Roho Mtakatifu ni Uwepo wa Mungu unaotuzunguka kila siku.
Kumbuka pale Yesu alipo sema
" Mungu ni Roho na wamuabuduo inabidi wamwabudi katika Roho na Kweli "
Hivyo Roho Mtakatifu ndio umbo la Mungu yaani Mungu ni Roho takatifu ila kwakuwa hiyo Roho ni hai na inatenda kazi basi inaitwa " Roho Mtakatifu" na sio "Roho Takatifu"
Inaitwa tena " Roho wa Mungu " na sio " Roho ya Mungu "

Hivyo basi Mungu huyu huyu mmoja ameitwa Baba, Yesu na Roho Mtakatifu kutokana na zile kazi zake kuu tatu alizomtambulisha mwanadamu,
Kazi ya uumbaji, = Baba.
Kazi ya Ukombozi, = Yesu Kristo.
Kazi ya kuwa nasi (msaidizi) wa kuendelea kutusaidia katika shida zetu = Roho Mtakatifu.

Nawasilisha.
 
MKUU umeitoa wapi hiyo habari
weka link
 
NIMEPATA kitu kizuri sanaaaa
muandishi wa hiyo kitu
alipataga wapi hayo maono
 
umenisisimua mahali
ndiyo maana nikawa nashangaa Y? ukitaja jina la YESU mapepo na mambo mabovu yanakimbia/kuweweseka?
lakini nikawa najiuliza Y? ukitaja jina la Mtume (Saw) yaani hata mapepo haya ropoki
asee hapo NIMEPATA kitu
 
MKUU haya madini umeyapata wapi?
tupeane kwa kweli
 
Muwasilisha umepewa upeo nzuri sana, na ni kweli kabisa Kuwa muumini mfuasi wa Dini Fulani bila makubaliano (wito wa kiteule) ni bure kabisa, Mungu lazima akuite yeye mwenyewe kwa mwaliko wake nafsini kwako ambapo wewe mwenyewe ndio utaukiri uungu wake kupitia hayo maono yako. Bila hivyo ndio inatokea kundi la walalamikaji na waamuzi.
 
Mkuu mimi naomba unipe link nienede nikaisome kwa lugha halisi ya mwandishi halisi tofauti na hii yako uliyotafsiri. Asante
 
umenisisimua mahali
ndiyo maana nikawa nashangaa Y? ukitaja jina la YESU mapepo na mambo mabovu yanakimbia/kuweweseka?
lakini nikawa najiuliza Y? ukitaja jina la Mtume (Saw) yaani hata mapepo haya ropoki
asee hapo NIMEPATA kitu
Mkuu umegusia jina la Yesu ningependa unisaidie jambo mfano Yesu kwa kiswahili ukienda nchi nyingine unakuta anaitwa Yashuah au uingereza utakuta ni JESUS.... Na kuna maeneo mengine duniani kama Asia Yesu au Jesus ina maana tofauti kabisa na wanatumia jina tofauti kumaanisha Yesu...

Sasa nachojiulizaga inayofanya kazi ni LILE jina la mwana wa Mungu tunalotaja kwa makabila Yetu au ni ile imani kichwani inayotengeneza connection kati ya sisi wanadamu na mwana wa Mungu (bila kujali anaitwa Yesu kiswahili au yashuah kiebrania)....

Naomba unisaidie ingawa nimetoka nje ya mada
 

Pingamizi zangu za kimantiki kuhusu uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa kiingereza "proof by contradiction", bado hazijapata majibu ya kuziondoa.

Hivyo, Mungu hayupo.

Kama mtu anasemayupo, athibitishe kwa kuanza kuondoa contradictions zilizopo katika habari ya kuwapokwake.


Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungub wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.
Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikanw vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Unaweza kujibu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…