Biden akubali kuipa Ukraine mabomu ya kutegwa ardhini

Biden akubali kuipa Ukraine mabomu ya kutegwa ardhini

5523

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2014
Posts
2,275
Reaction score
2,410
Vita inaingia kwenye sura nyengine

1.jpg


20 Novemba 2024
Rais wa Marekani Joe Biden amekubali kuipa Ukraine mabomu ya kutegwa ardhini, afisa wa Marekani ameiambia BBC.

Afisa huyo ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, anasema mabomu ya aina hiyo yatapelekwa hivi karibuni na Washington inatarajia yatatumika katika eneo la Ukraine.

Kyiv pia imeahidi kutotumia mabomu hayo katika maeneo yenye raia wa Ukraine, afisa huyo amesema.

Hatua hiyo inaonekana kama jaribio la kupunguza kasi ya wanajeshi wa Urusi ambao wamekuwa wakisonga mbele kwa kasi mashariki mwa Ukraine katika miezi ya hivi karibuni.
 
Kumbe Putin anapigana na watu ambao hawana uwezo wa land mine? Duuuu! Ni vichekesho sana
 
Democrats hawana na cha kupoteza tena baada ya kugaragazwa na warepublicans, sasa wanatamani wakose wote
 
Back
Top Bottom