Biden kabakiza miezi miwili mjengoni kaanza kumharibia nyumba mpangaji mpya, Kwa maksudi anaichochea vita ya Ukraine ili kumwangushia jumba bovu Trump

Biden kabakiza miezi miwili mjengoni kaanza kumharibia nyumba mpangaji mpya, Kwa maksudi anaichochea vita ya Ukraine ili kumwangushia jumba bovu Trump

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Trump aliapa atawekeza nguvu kubwa kuleta makubaliano ya kuituliza vita ya Ukraine na Russia, Siku chache baada ya kushinda uraisi, Putin rais wa Urusi alisema yupo tayari kwa majadiliano ya kuimaliza vita.

Hii imewauma sana Democrats, Kwamba Trump anaenda atajizolea points akiimaliza vita.

Kilichoanza ni mikakati ya kumwagia petroli moto unaozimika, Mpangaji aliepewa notisi ya miezi miwili kuondoka kumpisha mpangaji mpya kaanza kuchana singibodi, kuchafua rangi, kungoa vitasa, kubamiza fenicha, yote hii ni kisasi kwa mpangaji mpya.

Joe Biden (Nyuma yake wapo kina Obama) ameiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu ya Marekani, Jitihada zote hizi ni kuichochea vita.

Trump anaingia mjengoni vita imepamba moto, Itakuwa ni ngumu sana kupata suluhisho kwa njia ya Diplomasia
 
Russia aliivamia Ukraine bila kurushiwq hata jiwe!. Na hapo ni baada ya kuichukuwa Cremea. Ukorofi upo kremlin.
Umemeza habari za CNN, BBC na wengine bila kutafuna...
Mkuu ogopa sana media ukiwemo TBC!

Leo CNN wanasema Trump akifukuza wahamiaji bei za vyakula zitapanda bei maana vibarua wengi waliojiliwa mashambani ni wahamiaji wasio na "makaratasi" ya kuishi USA, ila kwa wale tunaofuatilia habari za uchumi Marekani kuna inflation ya kutisha hata kabla wahamiaji hawajaondoka, ila Jambo la kushangangaza nchi kama Marekani ambayo kilimo ni machines 99.9% vibarua ndio watikise sekta hiyo!
 
Biden kachukua ushaur aliopewa na trump baada ya kukutana kule white e house.., trump sio mtu wa kubembeleza kama Biden,alimchana Biden livelive siku Ile kwamba anaidekeza urusi,ndio maana unaona uamuzi huu Leo hii..,na kama hii hatua iliyochukuliwa na Biden Leo hii ingekuwa Haina baraka za Trump,basi republican members wengi wangekuwa wameshaibuka waziwazi na kumshutumu Biden, lakini mpaka Sasa unaona wote kimyaa! Kama hakuna kilichotokea vile
 
Umemeza habari za CNN, BBC na wengine bila kutafuna...
Mkuu ogopa sana media ukiwemo TBC!

Leo CNN wanasema Trump akifukuza wahamiaji bei za vyakula zitapanda bei maana vibarua wengi waliojiliwa mashambani ni wahamiaji wasio na "makaratasi" ya kuishi USA, ila kwa wale tunaofuatilia habari za uchumi Marekani kuna inflation ya kutisha hata kabla wahamiaji hawajaondoka, ila Jambo la kushangangaza nchi kama Marekani ambayo kilimo ni machines 99.9% vibarua ndio watikise sekta hiyo!

Habari karibu zote toka kwenye mainstream media zina agenda! Wamarekani si wajinga kiasi hicho kuunga mkono hoja ya kuwaondoa Wahamiaji haramu, wanajua negative impact yake! Mzigo wanaouleta kiuchumi na hata kijamii ni mkubwa kuliko faida yake!
 
Back
Top Bottom