Biden: Putin alijidanganya anaweza kusambaratisha NATO

Biden: Putin alijidanganya anaweza kusambaratisha NATO

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
USA Präsident Joe Biden Rede zur Lage der Nation

Rais Joe Biden wa Marekani amesema madikteta ambao hawawajibishwi kutokana na uchokozi wao ndio wanaosababisha machafuko zaidi na kuongeza kuwa uvamizi wa rais Vladimir Putin wa Urusi nchini Ukraine ulikuwa ni wa kupangwa na wala haukuchochewa

Rais Biden ameyasema hayo kwenye hotuba ya hali ya taifa aliyoitoa kwa bunge la Marekani. Biden amegusia pia umuhimu wa washirika wake wa Ulaya akisema muungano ulioanzishwa baada ya Vita vya Pili vya duniani ili kurejesha amani na ustahmilivu una umuhimu mkubwa pia katika kipindi hiki na kusema Putin alikosea sana kuamini angeweza kuugawanya ushirikiano wa NATO, kwa kukataa juhudi za kidiplomasia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kwa upande wake ametoa mwito kwa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunga mkono azimio la kulaani uvamizi huo wa Urusi, akisema ni wakati sasa wa kuchagua kati ya amani ama uvamizi, haki ama matakwa ya wenye nguvu, kuchukua hatua ama kufumbia macho. Amesema hayo kwenye mkutano wa dharura wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Aidha balozi wa Urusi kwenye Umoja huo Gennady Gatilov amesemaUkraine haina nia ya kujaribu kusaka suluhisho halali na la usawa kuhusiana na mzozo baina yao. Amesema hayo akiwa mjini Geneva, kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha nchini Lebanon.

Shrika la habari la Urusi la RIA, lilimnukuu Gutilov kwenye mahojiano hayo akisema Urusi inaunga mkono diplomasia na usawa, lakini kwa sasa hawalioni hilo na kuongeza huu ni wakati muafaka wa kondoa silaha za nyuklia mashariki na magharibi mwa Ulaya.

Mbali na Urusi, wanajeshi wa mataifa mengine yenye nguvu kinyuklia barani Ulaya, Ufaransa na Uingereza pamoja na Marekani, ambayo pia yanamiliki silaha nyingi za nyuklia miongoni mwa wanachama wa NATO wamepiga kambi barani Ulaya
 
Sawa walivamia.

Kwa hiyo kama marekani walivamia nchi hizo maana yake kwamba na putin ni halali kwake kuvamia ukraine ?

Akifanya marekani dhambi na sisi inakuwa halalia kwetu kwa vile kafanya marekani ?

Russia anahaki zote za kulinda mipaka yake zidi ya magaidi wa nato
 
Sawa walivamia.

Kwa hiyo kama marekani walivamia nchi hizo maana yake kwamba na putin ni halali kwake kuvamia ukraine ?

Akifanya marekani dhambi na sisi inakuwa halalia kwetu kwa vile kafanya marekani ?
tulia Unyolewe mkuu, putin hapigani vita katika nchi ya Ukraini ila yeye anafaya OPERATION MAALUM, kwaiyo kuweni wapole wewe na kibaraka wenzio (marekani pamoja na nchi wanachama wa NATO).
 
Warusi wa Magomeni Mapipa bado tu hawaoni kwamba Urusi inaingia shimoni kweli ujinga ni mzigo.
 
Wamalize sasa kelele zao huko ulaya, vita yenyewe hatuoni ni maneno watu kufa majeshi kuingia sijui pale.

Ata huyo mrusi hana nia ya vita ila bila suluhu ndio inaweza kua majeshi yake yamefika ukraine na kutoka ikachukua miaka ata 10.

Au nasema uwongo ndugu zangu... Ayaaa mwingine
 
Soko la Hisa la Moscow limekwama kufanyika - leo siku ya tatu - giii

Putin anadhoofika mno baada ya hii vita.

1 hour ago (05:57 GMT)

Moscow Exchange won’t resume stock trading on Wednesday: Cenbank​

Russia’s central bank kept stock market trading on the Moscow Exchange suspended for a third day in a row on Wednesday, but said it would allow a limited range of operations for the first time this week.
 
Sawa walivamia.

Kwa hiyo kama marekani walivamia nchi hizo maana yake kwamba na putin ni halali kwake kuvamia ukraine ?

Akifanya marekani dhambi na sisi inakuwa halalia kwetu kwa vile kafanya marekani ?

Hizo ndiyo akili za vichwa panzi. Wakikuelewa usiache kutuletea mrejesho.
 
Sawa walivamia.

Kwa hiyo kama marekani walivamia nchi hizo maana yake kwamba na putin ni halali kwake kuvamia ukraine ?

Akifanya marekani dhambi na sisi inakuwa halalia kwetu kwa vile kafanya marekani ?
Hapana, kinachotushangaza ni kwamba anaeongoza kusababisha machafuko duniani, ndio anajidai yuko mstari wa mbele kukemea wengine.

Watu wengi hawana ubaya na Ukraine, ni vile tu hawapendi double standards. Wakivamia NATO na shoga yake USA, hakuna kelele. Akivamia Russia, wao ndio wanaongoza kupiga kelele. Hiki ndicho tunachokipinga. Maana mchawi mkuu, ndio anajifanya yuko mstari wa mbele kupinga uchawi.

Mwisho kabisa, the world needs tha balance of power. Dunia haitakua salama kama kukiwa na kiranja mmoja ambae akiamua la kwake, hakuna wa kupinga. Na wengine wakiamua ya kwao, yeye anaingilia. Hatufurahii ubabe wa Putin, lakini ubabe wake ni muhimu sana katika kutengeneza balance of power na amani ya dunia kwa ujumla.

Gharama ya kuipata amani ya dunia ni kubwa mno, sometimes inabidi kumwaga damu ya wasio na hatia kama raia wa Ukraine. Ili next time, kabla mtu hajaleta uchokozi, awe anajua kabisa kutakua na consequences!

Adiós
 
Nakubaliana na mawazo yako mkuu kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom