Uchaguzi 2020 Bidhaa inapokuwa ngumu inatafutwa mbinu mpya ya kuiuza

Uchaguzi 2020 Bidhaa inapokuwa ngumu inatafutwa mbinu mpya ya kuiuza

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BIDHAA INAPOKUWA NGUMU KUUZIKA UNATAFUTA MBINU MPYA ZA UUZAJI

Leo alfajir natoka msikitini rafiki yangu Abdallah Kageta ambae ndiyo mwadhini wa sala ya Alfajir hapa msikitini kwetu huwa tuna kawaida ya kupeana taarifa za kampeni za uchaguzi zinavyokwenda kila asubuhi kabla ya kila mtu kuelekea kwake.

Huyu Kageta ndiye aliyenipigia simu usiku kiasi miaka mitano iliyopita kunitaarifu kuwa Prof. Ibrahim Lipumba anajiuzulu uenyekiti wa CUF kesho asubuhi.

Sikumuamini na kwa kujiamini kabisa nilimuonya asisambaze taarifa hizo za uongo.

Nilimfahamisha Kageta kuwa Lipumba ni rafiki ndugu namjua vyema.

Labda kwa ile heshima ya umri wangu kwake mimi nikiwa kaka mkubwa sana kwake hakunibishia tukaagana.

Sisi kata yetu ni ya Mzimuni na hii ilikuwa ngome kuu ya CUF tukizoa viti vyote kila uchaguzi ikawa CCM wamekata tamaa kabisa kupata chochote Mzimuni.

Hali hii ilibadilika baada ya wagombea wa ACT Wazalendo wote majina yao kukatwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.

Hivi sasa bila kutoka jasho Mzimuni inatawaliwa na CCM.

Leo asubuhi baada ya sala Kageta kanishika mkono hadi kwenye ukuta wa nyumba yangu ananionyesha posta ya mgombea udiwani wa Mzimuni Bwana Lyoto Manfred.

Kageta ananiambia, "Mgombea wa CCM Lyoto hali ngumu anaogopa kutumia rangi za kijani za CCM kaamua posta zake azichape rangi ya bluu."

Naitazama posta kwa kuikagua naam posta mgombea wa CCM lakini ile rangi ya kijana haipo badala yake naona rangi ya Cosmopolitan Football Club.

Hii sijui kama imepata kutokea siku za nyuma.

Ningependa sana kutegua kitendawili hiki cha mgombea kuikimbia rangi yake ya uenyeji na kuchukua rangi ya kigeni.

Hii inaashiria kitu gani?

Kuwa kijani imepoteza mvuto?

Picha: Pembeni ya posta ni mkutano wa mwisho wa CUF Mzimuni ulioitishwa kusheherekea ushindi Serikali za Mtaa uliohutubiwa na Prof. Lipumba.

20201024_134845.jpg
 
Bia yetu, we jamaa uwage unasoma uzi watu wakiposti kabla ya kujibu! Unajibuje uzi bila kuusoma aisee
 
Bia yetu,
Huna sababu ya kunihurumia ikiwa huruma yako ni kuwa niliyokuwa nayataka hayakutimia.

Alhamdulilah kila nililomuomba Allah kanipa na mengine sikumuomba lakini kanipa.

Mohamed Said ni huyo hapo chini:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors
(1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.

Bwana Bia,
Hii ni picha ya Mzee Mohamed Said mwenye majuto?
 

Attachments

  • SYKES BOOK ALL EDITIONS.jpg
    SYKES BOOK ALL EDITIONS.jpg
    52.5 KB · Views: 1
Mzee said hili jukwaa lako tu, wengine huturuhusiwi
Siunaona comments zangu huwa zinafutwa
Hili sio jukwaa la mambo ya kitoto, ukiona post yako imeondolewa ujue ina utoto mwingi.
 
Kageta ananiambia, "Mgombea wa CCM Lyoto hali ngumu anaogopa kutumia rangi za kijani za CCM kaamua posta zake azichape rangi ya bluu."
Ewaaaaaaa safi sana Mkuu MS
 
Bwana Manfred kaikimbia Kijani na hata Njano? ama kweli Spana zimepigwa.
 
CCM ni chana cha dhulma, waliomo ndani wanaona aibu, mioyo yao inawasuta wanakosa pakuzificha sura zao.
 
Back
Top Bottom