Bidhaa nyingi zinazotengenezwa na Watanzania hazina ubora, bei juu

Asiliatz

Member
Joined
Aug 16, 2018
Posts
96
Reaction score
131
Habari wakuu!

Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza, ipo mijadala na humu Kuna baadhi ya uzi zimegusia juu ya ubora na bei ya bidhaa zinazotengenezwa Tanzania Kama chanzo Cha watanzania wengi kukimbilia bidhaa za nje.

Tanzania kumeibuka bidhaa nyingi zinazotengenezwa na watanzania ama viwanda vilivyopo Tanzania katika siku za hivi karibuni kutokana na Sera ya "Uchumi wa viwanda".

Miongoni mwabidhaa zinazozalishwa kwa wingi Tanzania ni nafaka, juisi,soda, maziwa, Samani(fanicha),vifunashio,sabuni,mafuta ya kula,vipodozi,majiko ya mkaa,vyombo vya chakula,viatu,nguo,mashine(kusaga juisi,kufyatua tofali,nk),viungo vya chakula,mapambo,vilevi,vifaa vya umeme, n.k Kuna karibia 90% ya bidhaa muhimu zinazalishwa Tanzania 10% iliyobaki Ni kwenye vifaa vya elekroniki na bidhaa zingine za teknolijia kubwa ambazo bado hatujaingia huko au tunagusa gusa tu.

Hakika baada ya kusoma Aya hapo juu umegundua kunabidhaa zingine nimetaja lakini hujui au hujawahi kuiona made in Tanzania lakini amini zipo na watu wanapambana kuzileta mbele ya macho yako.

Baada ya utangulizi huo, Sasa niseme neno Si kweli bidhaa nyingi za kitanzania hazina ubora asiliatz .com tumelenga kuuza bidhaa za kitanzania kwenye tovuti yetu tumekua tukitafuta na kutembelea watengenezaji wa bidhaa hizi za kitanzania kiukweli sisi wenyewe tunazipenda na tunakuwa nashauku kuziweka kwenye tovuti yetu, pia tulichogundua kunaubunifu mkubwa Sana watanzania wanao kitu ambacho kinapelekea kutoa bidhaa nzuri na zenye viwango, baadhi unaweza kuziona kwenye tovuti yetu.

Tatizo tulilogundua sisi Kama asiliatz baada yakuzungukia baadhi yawatengenezaji wa bidhaa hasa mkoa wa mwanza ni namna yakujibrand(kuzipa muonekano biashara zao) na uwoga kufanya kazi na watu Kama sisi, hivyo hata Kama akijitahidi atumie social network mwenyewe anakwama muda sababu hanakundi kubwa la kumuwezesha ashughulikie Oda,malipo,matangazo na pia aendelee na uzalishaji. Pendekezo madalali wa bidhaa za kielekroniki nazamfanano huo kutoka nje wageukie fursa kwenye bidhaa za ndani(TZ), pia wazalishaji wabidhaa waangalie fursa kwenye tovuti Kama hii yetu asiliatz .com ndio zitakua mkombozi badala ya kutegemea tu kuuza kupitia social networks.

Kuhusu bei na weza sema nikweli baadhi ya bidhaa za Kitanzania zinakuwa na bei Sana hii nikwasababu ya ubora wa bidhaa zenyewe, sizani Kama kunatatizo hapa watu wanachochanganya nimuonekano, bidhaa za Tanzania hazina muonekano mzuri Sana, na hii nikutokana pia wazalishaji hawapati au hawatafuti huduma Bora za IT mfano kutengenezewa logo. Hivyo ningeshauri kampuni na watu wa IT kuchangamkia fursa kusaidia wazalishaji wa bidhaa za Tanzania sio kukimbilia tu kina Vodacom and the like.

HITIMISHO
Soko au masoko yakuuza bidhaa za Kitanzania mtandaoni ndio suluisho namba moja ya kukuza Uchumi wa viwanda Tanzania. Kwa dunia ya Leo bila kuchangamkia sekta hii ya E-commerce itakuwa vigumu Sana kutimiza lengo.
Alibaba .com imesaidia Sana China kukua kiuchumi wa viwanda wakati imeanzishwa kulikua Amna kitu unaweza kusearch mtandaoni kuhusu China ukakipata lakina Leo tuna import Sana bidhaa kutokana China kupitia Alibaba naweza sema 95% watanzania tunaagiza bidhaa nje kupitia e-commerce je sisi huko nje watu wataagiza bidhaa zetu kupitia Nini? au tuendelee kutumia site zao ambazo tayari zinasoko lao.?

Ni hayo tu kwa Leo.
 
Kuna mkanda niliulizia maonesho ya sabasaba kwa jamaa flan wanatengeneza kwa ngozi....
Bei 30k....
Sasa nikilinganisha na huu Diesel nilionunua 25k unazidi ule mara 100...

Bongo kuna vitu bei juu lkjn ubora sifuriiii
 
Kuna mkanda niliulizia maonesho ya sabasaba kwa jamaa flan wanatengeneza kwa ngozi....
Bei 30k....
Sasa nikilinganisha na huu Diesel nilionunua 25k unazidi ule mara 100...

Bongo kuna vitu bei juu lkjn ubora sifuriiii

Inaweza kuwa ulikua hauna muonekano mzuri. sababu nyingine, huwezi linganisha na makampuni makubwa saa zingine wanatengeneza vitu Kama sehemu ya matangazo Kama hao diesel wanaweza kugawa hata bure. Kumbuka biashara ndogo au inayoanza haiwezi kushinda Vita ya bei dhidi ya kampuni kubwa.
 
Ni rahisi kununua bidhaa online toka China ikafika Kigoma, etc, ila so rahisi kulipia bidhaa Dar na ikafika Kigoma.
Note: Huu ni mfano kwa mteja wa kawaida.
Ukiwasiliana na wauzaji wakubwa, mkakubaliana bei, ukimuuliza. Je utanisaidia kufanikisha usafiri? Anakwambia HAPANA, jukumu letu ni kuuza tu.
Hao Jumia, Kupatana, Soko, .... wamesajiki wauzajiwa wa vitu vilvile vya kawaida kama magari, saa, laptop, simu, hereni, .... Ukiulizia bati, cement, nyaya za uzio, n.k hupati muuzaji.
 

Nikweli swala la usafiri Ni changamoto na watu Kama sisi ndio jukumu letu kutatua hi changamoto sisi Kama asiliatz .com tunalifanyia kazi hili ilikusudi mtu akiagiza online mzigo umfikie mlangoni.

Changamoto ya bidhaa inatatuliwa kama sisi watanzania tukiamua kuanzisha e-commerce sites kwaajili yavitu ambavyo tunaona havipatikani mtandaoni.
 
E-commerce sites zipo nyingi tu, ila zote hazifanyi kazi ya kueleweka. Takribani zote zinawauzaji wa bidhaa wanafanana: mikoba, pochi, tv, simu, ...
Hakuna reviews, mzigo utafika lini?
Ni kawaida kukuta muuzaji mkubwa, na hana transporting partner company
 

Kweli kabisa watu waki gundua hili la usafiri,mitandao na customer care ndipo biashara zitarudi kwenye uhai. Bado watu wanazani ni kwa makampuni makubwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…