masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 16,207
- 14,343
Mwishoni mwa mwaka jana, baadhi ya bidhaa, hasa zile zinazotumika kupika vitu mbalimbali, zilikuwa na bei ya chini. Hata hivyo, mwanzoni mwa mwaka huu hadi mwezi wa tatu, bei ya bidhaa hizi zilikuwa zimepanda sana.
Naamini hasira nyingi za Wakenya zinaelekea kwenye mswada wa marekebisho ya kodi. Hata kabla ya mswada huu, bidhaa zilikuwa tayari zimeanza kupanda bei. Sasa, je, mswada wa marekebisho ya kodi ukipita itakuaje?
Kwa mfano, tunaingiza siagi kutoka Kenya ambayo ni bora sana. Kwa sasa, bei yake imepanda na haimiliki kabisa. Pia, icing sugar ambayo hatuzalishi nchini, tunaiagiza. Hadi mwezi wa tatu mwaka huu, bei yake kutoka kiwandani ilikuwa Tsh 60,000 kwa carton, lakini sasa ni Tsh 81,000 ikiwa hapo Trufoods kabla hata ya kuitoa nje ya geti.
Hizi ni baadhi tu ya bidhaa nyingi ambazo bei yake imepanda sana.
Kwa ladha, kwa mfano, fleva za vyakula za mls 50 kutoka kampuni maarufu Kenya zilipanda kutoka Tsh 1,800 hadi Tsh 3,000 kabla hujaitoa hapo Keekrok Road.
Hata sisi tutaathirika sana na ongezeko hili la bei, kwa sababu kodi kubwa hulipwa na mlaji wa mwisho. Kumbuka, tunaingiza bidhaa nyingi sana kutoka Kenya. Waokaji, nafikiri mlishaanza kuonja joto hili kuanzia mapema mwaka huu.
#Wakenya wana kila sababu ya kuandamana