Bidhaa zipi naweza kusafirisha kutoka China kuja Tanzania?

rakeyescarl

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2007
Posts
481
Reaction score
147
Wakuu habari za biashara,

Naomba kujua kama nina dola elfu kumi ni bidhaa zipi naweza kupeleka Tanzania kutokea China kwa njia yoyote ni sawa hata kwa ndege.

Kiwango cha faida nahitaji kama net=9%,ikiwezekana.

Kwangu ni rahisi kwa sababu nina mtu ambaye yuko pale.

Natanguliza shukurani.
 
Upakie mzigo kwa ndege kutoka china utabeba nini kil moja kwa ndege ni 40000 sasa utakuwa unafanya biashara au
 
Upakie mzigo kwa ndege kutoka china utabeba nini kil moja kwa ndege ni 40000 sasa utakuwa unafanya biashara au

Kazi kweli kwa bei hiyo...sasa wale wanaoenda kuchukua nguo kadhaa tu beg 3(ni mfano tu) huwa wanafanyaje maana kuupeleka kwa meli bado ni mdogo sana
 
Kazi kweli kwa bei hiyo...sasa wale wanaoenda kuchukua nguo kadhaa tu beg 3(ni mfano tu) huwa wanafanyaje maana kuupeleka kwa meli bado ni mdogo sana

Kuna agents wanaosafirisha mizigo kwa ndege toka China ni dollar 10 kwa kilo moja. UK ni paund 5 kwa kilo kama sijakosea.
Nilishawahi pokea wangu kwa hiyo njia.
Ila tatizo ni TRA pale airport huyo mtu wako asipokuwa makini wanakuunguza

Upakie mzigo kwa ndege kutoka china utabeba nini kil moja kwa ndege ni 40000 sasa utakuwa unafanya biashara au
 
Hata uwe na box moja door to door home shoping center wanakusafirishia tu

Nashukuru kwa taarifa hii...nafikiri unawafaham vema hawa watu,hivi wapo na Thailand,Philipine na Dubai maana safari yangu ya kwanza kwa kufanya manunuzi nimepanga iwe Thailand maana nasikia kule vitu ni bei rahisi zaid kuliko China..then kuna thread moja iliwekwa hapa wiki iliyopita kuwa hawa HSC ni kweli mzigo wanakufikishia ila hawakupi document za malipo ya ushuru na tax nyingine hivyo kukamatwa ni rahisi na wao hawahusiki japo unakuwa umewalipa gharama zote hizo,hizi taarifa ni za kweli kama umeshawahi fanya nao biashara..
 
Kumbe mkuu umejichimbia huku heeee makubwa?
kazi kweli kwa bei hiyo...sasa wale wanaoenda kuchukua nguo kadhaa tu beg 3(ni mfano tu) huwa wanafanyaje maana kuupeleka kwa meli bado ni mdogo sana
 
Hebu wacheki na hawa dhl ujue wao wanasafirisha mizigo kwa bei gani jua charge yao kwanza kabla hujadhurumiwa bure

heee ndo mambo ya mpunga yameiva mpaka wataka safiri mkuu hongera sana? (jokes)
umeshajisajiri na alibaba?
 
Siasa na hapa ndipo ninapopenda kupitia kidogo,I hope safari yenu imeiva maana ulitaka kwenda Thailand na wewe unaweza nipa mambo mengi kweli namna ya kusafirisha vimzigo,au umeahirisha sio December hii tena
 
lete laptops tufanye biashara
 
nimehairisha mwenzangu mpaka mwakani kwani mambo hayakaa vizuri kipesa nitaenda tu kwani tulishajioganize watu wa kwendaa huko ila mwenzetu dikembe yeye amekwenda labda muulize huyo mkuu atakwambia
Siasa na hapa ndipo ninapopenda kupitia kidogo,I hope safari yenu imeiva maana ulitaka kwenda Thailand na wewe unaweza nipa mambo mengi kweli namna ya kusafirisha vimzigo,au umeahirisha sio December hii tena
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hawa watu wapo DUBAI na CHINA(Guanzouh) tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…