SoC02 Bidhaa zisizo halisi (Genuine)

SoC02 Bidhaa zisizo halisi (Genuine)

Stories of Change - 2022 Competition

leekingroy

Member
Joined
Jan 6, 2016
Posts
5
Reaction score
2
UTANGULIZI
Tanzania ni nchi inayo pokea bidhaa nyingi sana ambazo si halali kutoka kwa watengenezaji bidhaa hizo kama vifaa vya umeme na nyenzo za kazi.


BIDHAA ZISIZO HALISI
Bidhaa nyingi zinazo ingia nchini kutokea China na maeneo mengine ulimwenguni asilimia kubwa sana huwa ni bidhaa zisizo halisi kutokea kwa watengenezaji halisi.

Mfano wa bidhaa hizo ni bidhaa za kutumia umeme, na kutokana na uhitaji mkubwa na soko huru, Tanzania huruhusu bidhaa hizo kuingia nchini hivyo kusababisha bidhaa zile halisi kutokuwa na thamani na kukosa soko.

Bidhaa nyingi zilizo madukani zinauzwa zikiwa katika ubora usio kidhi mahitaji ya mtanzania. Bidhaa za aina ya simu ni bidhaa zilizo jaa katika soko la Tanzania kwa gharama nafuu ila sio zenye viwango stahiki. Wasambazaji wa simu za mkononi zilizo halisi (genuine) hupata changamoto katika mauzo kutokana na soko la simu hizo kutekwa na simu ambazo sio halisi kwa kuwa na mfanano (copy) na zile halisi, hiyo inapelekea mauzo kuwa hafifu kwa simu halisi.

Pia kutokana na hali duni ya watanzania wengi kuwa wenye kipato cha chini, inapelekea kujikidhi kwa kununua simu za gharama nafuu ili kutimiza adhma yao ya kuwa na mawasiliano.

Bidhaa nyingi zinazo ingia nchini ni bidhaa za kutumika muda mfupi, yaani bidhaa zenye thamani ya muda mfupi na kutokana na kwamba wafanya biashara wamesha tambua hilo, wanatengeneza bidhaa zenye thamani ndogo tofauti na wanavyo zitangaza hivyo bidhaa hufika na kutumika kwa muda baada ya hapo hupoteza thamani yake na hivyo kutokuwa na thamani tena.

Vifaa vya umeme kama redio za mziki mkubwa (subwoofer) huuzwa kwa wingi sana na kutokana na bei kuwa ndogo, imepelekea redio zile za thamani kutokuwa kimbilio na hivyo watanzania kununua redio za kichina kukidhi majmhitaji ya mziki ikiwa thamani yake huisha mapema kwa kuwa huaribika kirahisi ili wanunue nyingine (mbinu ya kufanya wasidumu nazo muda mrefu).

Kutokana na hili, watanzania wengi hununua bidhaa kwa kuangalia bei na sio thamani na ubora wa bidhaa wanayo nunua. Hivyo hujutia baadae pale bidhaa inapo poteza thamani na ubora wake.

IMG_20220606_130229_8.jpg
 
Upvote 2
Pita na kwangu ndugu "vita ya vijana dhidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia"
 
Back
Top Bottom