Bifu Diamond na Ali Kiba ni miradi ya watu

Bifu Diamond na Ali Kiba ni miradi ya watu

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Baada ya kuanzisha mashindano ya mbio kati ya farasi(Dimond) na kobe(kiba) na kutaka kuiaminisha dunia kuwa kobe ana mbio kushinda farasi, hatimaye ile miradi iliyotangazwa kwa nderemo na vifijo imeanza miradi hiyo yote inaonekana ilibuniwa kwa ustadi kabisa kwa kumtumia kiba na mtu aliyepo juu katika game ili kusudi pesa zipatikane kwa watu hao.

Miradi hiyo ni pamoja na Tshirt zilizoandikwa Kiba ni mfalme wa muziki, Dimond mwisho Tandale mjini kote kiba, Cd zilizoandikwa Kiba V Dimond, kwa mtu yeyote mwenye akili atagundua kumbe lile zomeazomea na mambo ya ajabu kama Dimond eti alisema mbeya hamna hoteli ya yeye kulala ilikuwa ni mipango ya watu wachache ya kutengeneza hela, laiti ingekuwa siasa ungesema ni siasa za maji taka, Kumbe hili bifu la kupikwa lilianzishwa ili watu fulani wapate hela na kwa uhunguzi wangu hawa watu wanajiita Team kiba.

Imani yangu ni kwamba mashabiki wa Kiba wapo tena wastaarabu lakini hizi hype zilizoanzishwa za Kiba V Dimond ni kwaajili ya manufaa ya watu wachhache ambao kwa maslahi yao wanataka kumchafua "Chibu Dangote" ili waje kutuuzia Tshirt na Cd zao uchwara ,kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuvaa Tshirt imeandika Dimond mwisho Tandale!!!

Tussuport muziki mzuri...

nawasilisha
 
Du…!!! Tz ni sheeeeedaaaahhh kama tumefikia hapa kamwe muzik wetu hautoweza kusonga na kama kiba mwenyew anakubal kifanya hv bas hakika siwez kusikiliza muzk wake hata mmoja endapo nitathibitisha tu, na hawez kupona kamwe katika muzik na mwisho wake ndio utakuwa huo.
 
Wewe ni mmoja wa watu wanao kuza haya mambo na hutaki yaishe na unataka yaendelee!

Hebu anza wewe kuacha kupandikiza chuki kwanza wengine watafuata!
Nyie ambao hamuwezi kuandika chochote kwenye topic bila kuwalinganisha Kiba na diamond ndio mnao eneza chuki baini yao na sijui mnapata faida gani!

Uwezi kuwasilisha mada kwa kukashifu msanii mwingine na bado utegemee chuki isiendelee kusambaa!

Hebu wewe onesha mfano kwa kujaribu kuandika mambo mazuri kuhusu wao bila kujaribu kuwachonganisha kwa kumkashifu mmoja wao!

Nyie mnao kwenda kwenye show zao kila Leo ndio mnajiweka kwenye hatari maana mnapo elekea mta mwagiana tindikali!

Mgejua hizi habari zenu za Kiba vs Diamond zina chosa na zimeanza kukera na mtawachonganisha kweli mnapo elekea!

Haya mambo yenu ya Kiba vs Diamond yanafanya hata watu washindwe kuwakosoa maana wataonekana wana chuki kumbe sivyo!

Hebu anzeni kutumia nguvu nyingi kuwapatanisha kuliko kuendeleza huu utoto bhana!
 
kwa iyo kiba aache kufanya muziki eti kwA kua dimond yupo juu?hakuna vya hivyo bhana.
 
wewe naye ni wale wale wasakaTonge una tofauti gani na hao umaowasema?? una maana gani kusema Diamond ni Farasi na Kiba ni Kobe?? huoni kama unaendeleza yale yale unayoyakataa??
 
wewe naye ni wale wale wasakaTonge una tofauti gani na hao umaowasema?? una maana gani kusema Diamond ni Farasi na Kiba ni Kobe?? huoni kama unaendeleza yale yale unayoyakataa??

Dimond yupo juu kwenye game hili hata asiyeona wala kusikia anajua ...

Ni sawasawa umlinganishe JB na Bishanga wa mambo hayo
 
Dimond yupo juu kwenye game hili hata asiyeona wala kusikia anajua ...

Ni sawasawa umlinganishe JB na Bishanga wa mambo hayo

Kiba na Diamond wote wako level moja tu hakuna anayemzidi mwenzake
 
Hii issue ni kama ya Messi vs Ronaldo,, kila mtu hua anamsifia ampendae,,,,bt ndo ushabiki ulvo,,,na tusitegemee mambo haya kuisha bcz wanapokuwepo wawili ambao nibora huu mvutano hua upo tu,,,na upo kwa mashabik,, cdhan kama wahusika wanawazia sana mambo haya..
 
Hamna kazi za kufanya wenzenu wanapiga hela niue mmekalia ubishi nani zaidi wakipita kwenye magari yao hata hawakujui kam JF unatoka povu kuwatetea
 
Wewe ni mmoja wa watu wanao kuza haya mambo na hutaki yaishe na unataka yaendelee!

Hebu anza wewe kuacha kupandikiza chuki kwanza wengine watafuata!
Nyie ambao hamuwezi kuandika chochote kwenye topic bila kuwalinganisha Kiba na diamond ndio mnao eneza chuki baini yao na sijui mnapata faida gani!

Uwezi kuwasilisha mada kwa kukashifu msanii mwingine na bado utegemee chuki isiendelee kusambaa!

Hebu wewe onesha mfano kwa kujaribu kuandika mambo mazuri kuhusu wao bila kujaribu kuwachonganisha kwa kumkashifu mmoja wao!

Nyie mnao kwenda kwenye show zao kila Leo ndio mnajiweka kwenye hatari maana mnapo elekea mta mwagiana tindikali!

Mgejua hizi habari zenu za Kiba vs Diamond zina chosa na zimeanza kukera na mtawachonganisha kweli mnapo elekea!

Haya mambo yenu ya Kiba vs Diamond yanafanya hata watu washindwe kuwakosoa maana wataonekana wana chuki kumbe sivyo!

Hebu anzeni kutumia nguvu nyingi kuwapatanisha kuliko kuendeleza huu utoto bhana!

asante
umeongea yote
km ana akili ht ya kuvaa boksa yeyote mpenda kupandikiza chuki ataacha akishasoma maandishi yako
 
asante
umeongea yote
km ana akili ht ya kuvaa boksa yeyote mpenda kupandikiza chuki ataacha akishasoma maandishi yako

Tumechoka huu ubishani kwa kweli...tuachane na hizo habari tujadili mambo mengine....sisi tuna thread yetu tutajadiliana kivyetu na wao wafungue yao
Anapenda sana ugomvi huyu sijui ni mtu wa dizain gani elnino
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom