Bifu la Jide na Ruge, nani anaumia zaidi?

Bifu la Jide na Ruge, nani anaumia zaidi?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kwa mtazamo wangu rahisi naona mgogoro huu ukimnyayua zaidi Jide kutoka utukufu hadi utukufu huku ukimuacha Ruge akijengea maadui.wengi zaidi, na wafuasi wake wakionekana ni wasaliti na wakandamizaji na wanyonyaji wa haki za wasanii.
Je wewe unaona nini kwenye mgogoro huu?
 
Ni kweli lakini pia hata Jide naye anaathirika kwa namna ileile ya Ruge kinachomfanya Jide aonekane anafaidika zaidi na huu mzozo ni kwakuwa biashara zake nyingine hazihusiani na tasnia ya muziki moja kwa moja ila kwa Ruge anaathirika zaidi kwakuwa karibu biashara zake zote tunazozijua zinahusika na wasanii moja kwa moja mfano Radio Tv na matamasha mbalimbali anayoandaa
Lakini pia Ruge amekuwa akilalamikiwa Siku nyingi kuwanyonya wasanii na kuwagawa ili aweze kuwatumia vizuri zaidi.shida iliyopo ni kuwa hakuna mpaka sasa aliye tayari kuwaweka chini wawili hawa na kuwasikiliza hoja na malalamiko yao ,zaidi sana Jide katoa waraka na Ruge kakimbilia mahakamani
Angalizo; Jide kama Jide naye anamatatizo yake anapata sympath kwasasa kwakuwa tu Ruge tayari alishawekewa vinyongo na wengi na sasa wamepata past kutolea nyongo zao baada ya Jide kuanza
Hatari iliyopo mbele ni kwamba Jide hatakuwa kufanya mziki na mwanamuziki mwenye mahusiano na clouds Tv na Redio vilevile Ruge naye hatakuwa tayari kufanya kazi na mtu mwenye mahusiano na Jide sasa hapo utaona wote watakavyoathirika kibiashara
 
Jide anazidi kupanda chati, japo co mpenzi wa bongo fleva, lakini show yake nimeikubali na nitakuwepo. Big up jide.
 
Team anaconda ndo habar ya mujini,jana dj faty kamsifia fa facebook ndani ya mda mchache comment kibao na sapport kwa jide,mwenyewe kaifuta,aibu yao
 
When you are small and your enemy is big, your enemy is exposed while you are hidden, you are mobile and your enemy is slow...all in all, japo wote wanadisadvantage but Ruge ana pata hasara zaidi...his PR is highly damaged.
 
Hili bifu ni mwanzo wa kifo cha kifo cha Clouds Fm, ninaona kabisa shika dogo likiuangusha mbuyu
 
Signora la Vechia. Clouds wanasemwa sana kuwanyonya wasanii wa bongo ila cha ajabu hao wasanii wenyewe hawalalamiki kama wanaonewa. Washabiki wanavyotokwa na mapovu kama wao ndio wanafanya sanaa. HAKIELIMUUU. Stuka
 
Ni kweli lakini pia hata Jide naye anaathirika kwa namna ileile ya Ruge kinachomfanya Jide aonekane anafaidika zaidi na huu mzozo ni kwakuwa biashara zake nyingine hazihusiani na tasnia ya muziki moja kwa moja ila kwa Ruge anaathirika zaidi kwakuwa karibu biashara zake zote tunazozijua zinahusika na wasanii moja kwa moja mfano Radio Tv na matamasha mbalimbali anayoandaa
Lakini pia Ruge amekuwa akilalamikiwa Siku nyingi kuwanyonya wasanii na kuwagawa ili aweze kuwatumia vizuri zaidi.shida iliyopo ni kuwa hakuna mpaka sasa aliye tayari kuwaweka chini wawili hawa na kuwasikiliza hoja na malalamiko yao ,zaidi sana Jide katoa waraka na Ruge kakimbilia mahakamani
Angalizo; Jide kama Jide naye anamatatizo yake anapata sympath kwasasa kwakuwa tu Ruge tayari alishawekewa vinyongo na wengi na sasa wamepata past kutolea nyongo zao baada ya Jide kuanza
Hatari iliyopo mbele ni kwamba Jide hatakuwa kufanya mziki na mwanamuziki mwenye mahusiano na clouds Tv na Redio vilevile Ruge naye hatakuwa tayari kufanya kazi na mtu mwenye mahusiano na Jide sasa hapo utaona wote watakavyoathirika kibiashara
Hilo litawezekana endapo clouds fm itaendelea kuwa na influence kwa wasanii,otherwise this is the very great opportunity for other company to take over!just watch and you will see!
 
Wote ni wafanya biashara wazuri sana wanaojua kutumia kila fursa inayokuja mbele yao vizuri sana. Hata hivyo, wote wameshindwa kuelewa kuwa, negativity na uncertainity yoyote huwa siyo nzuri katika biashara. Mgogoro baina yao unawajengea sehemu fulani ya negativity ambayo wanatakiwa kuiepusha kwenye biashara zao. Baada ya kuwakaruzana kidogo, wangekaa kitako na kujadili tofauti zao wakamalizana kimya kimya na kuwatangazia wafuasi wao kuwa hakuna tatizo baina yao kuliko kuacha tofauti hizo ndizo ziwatofautishe wafuasi wao pia.
 
Hii ni vita ya Times fm dhidi ya Clouds fm Jide ni chambo tu!
 
Hii ni vita ya Times fm dhidi ya Clouds fm Jide ni chambo tu! Times wanahamu ya kuwapokea kijiti Clouds ndo mana wameanza kuandaa matamasha sehem mbali mbali bila ya viingilio ikiwa ni matayarisho ya kuharibu Fiesta, subirin mtathibitisha! Kama ishu ni kupambana na wanyonyaji lini P funk alitubu dhambi ya unyonyaji kiasi cha kumsajili kwenye jeshi la ukomboz wa wasanii!
 
Ni kweli lakini pia hata Jide naye anaathirika kwa namna ileile ya Ruge kinachomfanya Jide aonekane anafaidika zaidi na huu mzozo ni kwakuwa biashara zake nyingine hazihusiani na tasnia ya muziki moja kwa moja ila kwa Ruge anaathirika zaidi kwakuwa karibu biashara zake zote tunazozijua zinahusika na wasanii moja kwa moja mfano Radio Tv na matamasha mbalimbali anayoandaa
Lakini pia Ruge amekuwa akilalamikiwa Siku nyingi kuwanyonya wasanii na kuwagawa ili aweze kuwatumia vizuri zaidi.shida iliyopo ni kuwa hakuna mpaka sasa aliye tayari kuwaweka chini wawili hawa na kuwasikiliza hoja na malalamiko yao ,zaidi sana Jide katoa waraka na Ruge kakimbilia mahakamani
Angalizo; Jide kama Jide naye anamatatizo yake anapata sympath kwasasa kwakuwa tu Ruge tayari alishawekewa vinyongo na wengi na sasa wamepata past kutolea nyongo zao baada ya Jide kuanza
Hatari iliyopo mbele ni kwamba Jide hatakuwa kufanya mziki na mwanamuziki mwenye mahusiano na clouds Tv na Redio vilevile Ruge naye hatakuwa tayari kufanya kazi na mtu mwenye mahusiano na Jide sasa hapo utaona wote watakavyoathirika kibiashara

Very good analization mkuu. mshana
 
Last edited by a moderator:
Clouds haitaathirika chochote na kama ingekuwa ni kuathirika wangeathirika wakati wa mgogoro wao na SUGU!! Jide kwa sasa ananunfaika coz' anapata public sympathy na hii itasaidia sana kwenye show yake to the point hata kama ingekuwa ni uwanja wa taifa, angejaza tu! Hata hivyo, hili ni la kupita tu kwani linachangiwa sana na dasturi ya wana-Darisalama na Watanzania kwa ujumla....ni watu wa matukio! Habari ya mujini kwa sasa ni Jide vs Clouds, haya yatapita na si ajabu yasifike hata mwishoni mwa July; Jide atasahaulika na wana matukio kujikita kwenye matukio yaliyo hot!

Jide akitaka kunufaika, ni kabla huu upepo haujapita, anatakiwa kufanya show nyingi iwezekanavyo! Aende Mwanza, Arusha, Mbeya na miji mingine!! Narudia, huu ni upepo tu; JIDE atasahaulika na Clouds wataendelea kuwepo!! By the way, wadau wakubwa wa Clouds ni Wafanyabiashara wakubwa wanaopeleka matangazo pale ambao wala hawana muda wa kusikiliza ujinga unaondelea kwenye mitandao ya kijamii!!

Kuhusu kwamba Clouds watakimbiwa na wasanii, mnajidanganya!! Kila msanii anapenda kazi zake zipigwe Clouds; msizani kwamba haya yanayotokea sasa ndo yatawafanya wasanii wasipeleke kazi zao Clouds! Tuhuma dhidi ya Clouds hazijaanza leo! Kwa wasiofuatilia muziki wanazani hii ndo mara kwanza lakini wanaofuatilia tuhuma dhidi ya Clouds zimeanza miaka kadhaa iliyopita! Tuhuma dhidi ya Clouds zilianza hata kabla ya Sugu hajaanza kuwachana, in fact more than five years ago; lakini bado wasanii wanaendelea kupeleka kazi zao pale!! Hutaki unaacha, lakini Clouds wanaifahamu entertainment industry, wengine wote wanajaribu ili wawe kama Clouds. Na kutokana na ukweli huo, ndio maana msanii nyimbo yake isipopigwa radio station nyingine, husikii maneno lakini isipopigwa Clouds, tayari issue wakati ukweli ni kwamba Radio Station zote, narudia RADIO STATION ZOTE zinabana!!! Haya ya Jide na Clouds wengi wetu tunadandia treni tusiyojua inakotokea wala inakoelekea matokeo ndo haya unakuta hata mtu kama SUGU nae amejiingiza huku akiamini kwamba ni mapambano dhidi ya hujuma kwa wasanii unless kama nae ameamua tu kununua kesi kwavile ana bifu na Clouds na hivyo kuamua kumuunga mkono yeyote atakayetangaza vita na Clouds bila kujali dhima ya vita husika!!
 
Back
Top Bottom