Big results now: Kawambwa fanya hivi.....

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tatizo kubwa kuliko yote kwenye elimu ya Tanzania ni upungufu wa rasilimali watu na vitu kunzia shule za awali hadi vyuo vikuu. Mfano, vyuo vikuu vyetu vyote havina walimu wa kutosha na wenye sifa. Vyuo vingi vinaendeshwa na tutorial assistants, Assistant lecturers na lecturers zaidi kiliko maseniors na maprofs, Hivyo utakuta mwalimu mwenye digrii moja anafundisha mwanafunzi anayetafuta digree ya kwanza (undergraduates). Mwalimu mmoja anazuunguuka kufundisha vyuo vitatu achilia mbali kufundisha somo zaidi ya moja. Hivi walimu wa aina hii watatoa matokeo makubwa yapi? Shule na vyuo havina vitendea kazi, mfano, mwalimu aliyesoma na kumaliza shule au chuo bila ya kutumia maabara alipokuwa mwanafunzi ataweza kuitumia maabara kuwafundishia wanafunzi wake hata kama itajengwa shuleni kwake?

Ushauri wangu kwako Mh. Waziri ni kwamba, kuanzia leo hakikisha kuwa hakitolewi kibali kipya cha kuanzisha shule wala chuo kwa kipindi cha miaka 10 mfurulizo ili taifa lijenge uwezo wa kusomesha wataalamu wengi na mahiri katika fani ya kutoa mafunzo ili kuimarisha ubora wa shule na vyuo vilivyoko sasa kwanza. Vinginevyo shule na vyuo vitaendelea kunyang'anyana walimu waliopo wasiotosha, na shule na vyuo vinavyoumia zaidi ni vile vya serikali ambavyo mishahara yake ni midogo kulinganisha na private na kusababisha walimu waende shule za private ama kuajiriwa au kufanya part-time huku
wakiacha vyuo vya serikali bila walimu wa kutosha na mahiri. Zoezi la kujenga maabara kwnye shule liende sambamba na kusomesha walimu wa sayansi na watu wa maabara kuwapa ujuzi wa namna ya kutumia maabara hizo, vinginevyo walimu watazikodolea macho tu kwakuwa wao walisoma bila ya kutumia maabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…