Qualifier
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 1,252
- 405
Sijui kama ni shule zote lakini baadhi ya shule za msingi za wilaya ya Kilombero hasa zilizopo Ifakara mjini zime anza mkakati wa kutoa matokeo makubwa sasa (Big results now ) kwa kurudia kuwachangisha wazazi Tsh.45,000/= bila kutoa risiti na baadae Tsh. 7000/= jambo lililo wafanya wazazi wa wanafunzi hasawa darasa la saba kuchangia jumla ya Tsh. 52.000/= kwa mwaka huu swali langu huu mpango wa big rusults now sasa unalenga kufungua miradi au kongeza usimamiaji wa walimu wakuu kuhakikisha walimu wanafundisha ipasavyo? je afisa Elimu ametoa elimu ya kutosha kwa wazazi ili wajue kuwa big results now itawagharimu wazazi bila kikomo? kwanini asishauri walimu wakuu watoe risiti za serilali ambazo wakaguzi wa hesabu wanaweza kukagua huu mpango ? na kwanini wazazi wapewe maagizo kabla ya kuelimishwa juu ya mpango huu ubora wake na gharama zake?