KALOKAGATHOS
Member
- Jul 9, 2013
- 38
- 6
Sera ya waziri mkuu wa Malaysia ilikuwa nzuri hususan katika mandhari ya Malaysia,mpaka kufikia anatangaza mpango wake huo wa kuikomboa nchi yake kimaendeleo,utafiti umefanywa wa kutosha,jopo la wataalam lilikaa likatafakari kwa kina na kwa wakati,likaona mapungufu,likatoa mapendekezo,sasa ni utekelezaji.Lakini huku Bongo kama ilivyo ada,kupakua na kupakia,wameibeba sera hii na kuibandika katika mazingira hatarishi kana kwamba Tanzania ya leo imekuwa Malaysia.Hata kama wote tulitawaliwa na Malkia,ndo kusema wote tunafanana?,kiuchumi hatuendani,viwango wa rushwa hatulingani,tena hapo tumewapiga gepu kubwa sana,unajua Malaysia kuja kuifikia Tanzania kwa viwango vya ufisadi ni baadae sana,labda miaka 200 ijayo,huku kodi za walala hoi ni vocha za mafisadi tena za kuongea na mahawara zao,sasa maendeleo yatatoka wapi?..Au mnadhani kuona majengo mengi ya Dar ndo ishara ya maendeleo? vipi kuhusu maisha ya mtu mmoja mmoja?,waingereza wanaita "per capita income"...hebu linganisha na ya Malaysia halafu uniambie BRN.