Mwaiona diploma ya ualimu inavyoendeshwa,
kwa kawaida kuhitimu mafunzo ni miaka miwili.Lakini kwa sasa hata mwaka hawamalizi wanakuwa wameisha hitimu.
mfano walioingia mwaka 2008/2009,waliondoka chuo mwaka jana mwezi wa tano,wakielekea BTP yaani kwenye mazoezi ya kufundisha mashuleni.walikaa huko miezi kama 4 tu.Waliambiwa warudi majumbani kwao hadi mwaka 2009 mwezi wa 4 tayari kufanya mtihani wa kuhitimu diploma yao.
Kwa hiyo kwa kifupi diploma wanaisomea si zaidi ya mwaka mmoja,kwani mwaka wa pili wote wanakuwa makwao.
Walioingia 2009/2010,
Nao walianza mwezi wa tisa mwaka jana,kwa sasa wako BTP hadi mwaka 2010 mwezi wa 4 watakuja kufanya NECTA.Kwa kuhesabu hao wamesoma kwa muda wa miezi 5 tu.
HIYO NI DIPLOMA YA UALIMU KWA MIAKA HII.JE elimu inaenda wapi?