Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,415
Habari wana JF?
Wiki moja iliyopita nilikuwa Moshi, nilikutana na mama amabaye alikuwa jirani yetu miaka ya 80 hadi 90 mwishoni, tulipiga sana story na akanikumbusha tukio la kuonekana Bikira Maria (Mama wa Yesu) kwenye mlima Kilimanjaro mwaka 90.
Kilichomfanya akumbuke ni kwamba mimi binafsi sikuwahi kumuona huyo Bikira Maria hapo mlimani kwa macho yangu ingawa nilikuwa naangalia kwa bidii zote, huyu mama alikuwa anamuona pamoja na wengine wengi wakati huo na hivyo akasema asiyemuona Bikira Maria basi ana dhambi na atakufa soon.
Nililia sana siku hiyo na siku kadhaa za tukio hilo maana wenzangu wote walikuwa wanamuona ila mie mpaka habari hizo zinaisha sikuwahi kumuona hata siku moja. Kwa hali hii nikajikuta nakumbuka tukio hili kubwa la kihistoria liliowahi kutokea Moshi na inaonekana limesahaulika kabisaa katika jamii yetu
Lilikuwa ni tukio lilifanya mji wa Moshi kuzizima na macho ya wakazi wake kuelekea Mlima Kilimanjaro kumuangalia Bikira Maria, wapo wanaodai walimuona na wengine kama mimi hatukumuona.
Walowahi kumuona wanadai (akiwepo huyu mama) walimuona mama wa Kizungu kajitanda kama jinsi picha za Virgin Mary zinavyokuwa na alikuwa anaonekana kama anafanya maombi vile. Pia kuna siku nyingine alikuwa anaonekana kichwa tu kwenye barafu za kilele cha mlima na alikuwa akigeuka huku na huko (hafanyi maombi).
Humu tumo wengi na naamini wakati wa tukio hili kuna watu humu wanaweza kuwa walikuwepo, walishuhudia au walisikia chochote kutokana na tukio hilo la wakati huo.
Hebu tukumbushane hili tukio na mwisho wake ilikuwa ni nini hasa?? Maana mie binafsi nilikuwa bado kijana mdogo na sikumbuki liliishia wapi.
Nawasilisha