BIL 18. 5 kusambaza umeme K'njaro

BIL 18. 5 kusambaza umeme K'njaro

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
SHIRIKA la umeme nchini(Tanesco),limetoa shilingi Bilioni 18.5 kwa ajili ya utekelezaji wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 135 vya mkoa wa Kilimanjaro .

Utekelezaji huo utafanywa na mkandarasi CEYLEX ENGINEERING CO. LTD kwa muda wa miezi 24 kuanzia sasa.

Mkurugenzi wa fedha wa Tanesco,Daniel Mungure alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Nurdin Babu wakati akimtambulisha mkandarasi huyo.

Alisema mkoa wa Killimanjaro wenye vijiji 519,vijiji 506 vina umeme na vijiji 13 havina umeme huku vitongoji 182 vikiwa kwenye hatua ya utekelezaji kwa kuwa na wakandarasi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 135 vya mkoa wa Kilimanjaro kati ya vitongoji 161 ambavyo havina umeme.

Mbali na umeme,Tanesco pia ipo katika mpango wa kusambaza mitungi ya gesi 452 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku ya aslimia 50 pamoj na kusambaza maiko banifu kwa magereza yote ya mkoa wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na vituo vya JKT kwa nchi nzima.

Alisema kuna miradi mingine inaendelea kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya walitoa Bilioni 1.7 kwa ajili ya migodi midogo,vituo vya afya viwili pamoja na Pumpu za maji.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilmanjaro ,Nurdin Babu amesema maono ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuona watanzania wote wanapata nishati ya umeme wa uhakika.

Alsema Rais amekuwa kinara namba mojo pia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia ndani na nje ya nchi na kuwataka Tanesco kuwafikia Mama Lishe na Baba lishe ambao wamekuwa wakitumia kuni kwa muda mrefu.

Mbali na hao,mkuu wa mkoa alitaka nishati hiyo safi isambazwe kwenye magereza na shule za sekondari za bweni ambako matumizi ya Kuni ni makubwa sana.

Akatoa rai kwa Tanesco kuhakikisha vitongoji vyote vinapata umeme na kuondoa manung,'uniko ya wananchi ambao vitongoji vyao havina umeme licha ya nyaya za umeme kupita kwenye maeneo yao.
 
SHIRIKA la umeme nchini(Tanesco),limetoa shilingi Bilioni 18.5 kwa ajili ya utekelezaji wa kusambaza umeme kwenye vitongozi 135 vya mkoa wa Kilimanjaro .

Utekelezaji huo utafanywa na mkandarqsi CEYLEX ENGINEERING CO. LTD kwa muda wa miezi 24 kuanzia sasa.

Mkurugenzi wa fedha wa Tanesco,Daniel Mungure alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Nurdin Babu wakati akimtambulisha mkandarasi huyo.

Alisema mkoa wa Killimanjaro wenye vijiji 519,vijiji 506 vina umeme na vijiji 13 havina umeme huku vitongoji 182 vikiwa kwenye hatua ya utekelezaji kwa kuwa na wakandarasi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 135 vya mkoa wa Kilimanjaro kati ya vitongoji 161 ambavyo havina umeme.

Mbali na umeme,Tanesco pia ipo katika mpango wa kusambaza mitungi ya gesi 452 itakayouzwa kwa bei ya ruzuku ya aslimia 50 pamoj na kusambaza maiko banifu kwa magereza yote ya mkoa wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na vituo vya JKT kwa nchi nzima.

Alisema kuna miradi mingine inaendelea kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya walitoa Bilioni 1.7 kwa ajili ya migodi midogo,vituo vya afya viwili pamoja na Pumpu za maji.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilmanjaro ,Nurdin Babu amesema maono ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuona watanzania wote wanapata nishati ya umeme wa uhakika.

Alsema Rais amekuwa kinara namba mojo pia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia ndani na nje ya nchi na kuwataka Tanesco kuwafikia Mama Lishe na Baba lishe ambao wamekuwa wakitumia kuni kwa muda mrefu.

Mbali na hao,mkuu wa mkoa alitaka nishati hiyo safi isambazwe kwenye magereza na shule za sekondari za bweni ambako matumizi ya Kuni ni makubwa sana.

Akatoa rai kwa Tanesco kuhakikisha vitongoji vyote vinapata umeme na kuondoa manung,'uniko ya wananchi ambao vitongoji vyao havina umeme licha ya nyaya za umeme kupita kwenye maeneo yao.
Pesa za kusambaza umeme zinatokana na sisi watumiaji wa umeme kukatwa kwenye kila malipo ya umeme tunayoyafanya, ninauhakika mama Samia hahusiki.
 
Imekuaje tena wakati nasikia wachaga walishasambaza umeme mpk vijijini toka 19... haya masambazaji mema ya umeme huko kilimanjaro
Nawasalimia wilaya ya hai kwasadala boma na masama mula
 
Hapa kutakuwa na upigaji,hakuna kijiji Kilimanjaro hakina umeme
 
Imekuaje tena wakati nasikia wachaga walishasambaza umeme mpk vijijini toka 19... haya masambazaji mema ya umeme huko kilimanjaro
Nawasalimia wilaya ya hai kwasadala boma na masama mula
Bado vijiji 13 tu kati ya 519. Vijiji vilivyobaki vipatiwe umeme haraka sana, umeme ni haki ya kila mmoja!
 
Imekuaje tena wakati nasikia wachaga walishasambaza umeme mpk vijijini toka 19... haya masambazaji mema ya umeme huko kilimanjaro
Nawasalimia wilaya ya hai kwasadala boma na masama mula

Wewe umeambiwa hapo kati ya vijiji 519, ni vijiji 13 tu havina umeme. Kafuatilie pia hivyo vijiji 506 vyenye umeme unaweza kuta zaidi ya 75% ni wananchi wamechanga wakajipelekea wenyewe.
Uliza mkoa wowote Tanzania wenye hiyo takwimu......
 
Back
Top Bottom