Bila cheti cha afya akili ndoa isifungwe!

Bila cheti cha afya akili ndoa isifungwe!

JEJUTz

Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
75
Reaction score
197
Kabla ya ndoa kufungwa,watarajiwa hulazimika kufanya vipimo vya afya zao hususan ukimwi.Hii imekuwa ni kanuni na imezoeleka hivyo.

Kutokana na yanaondelea huko ndoani watu kufanyiani mambo ya ajabu,kujeruhiana,kudhalilishana na hata wengine kutoana uhai.

Nashauri mamlaka husika ziweke sheria kuwe na ulazima sasa wa wanandoa watarajiwa kupima afya zao za akili kabla ya kuoana na kuanza kuishi pamoja.

Na itakapothibitika mmoja kati yao ana magonjwa ya akili,basi ndoa isifungwe ili kuepusha kadhia nilizoanisha hapo juu.

Ndoa ni jambo jema hivyo watu wanatakiwa waishi kwa upepo na amani. Ukichunguza vizuri utagundua kuna watu hawakupaswa kuoa ama kuolewa kwa namna akili zao zilivyo.


JJTz
 
Hili la akili za wanandoa ni bora ikawa hivyo kama ukimwi ili kuepuka majanga na ndoa kuvunjika. Unakuta mtu anaingia/anaingizwa ndoani huku hana akili za kuishi maisha ya ndoa, anaishia kuharibu ndoa mapema tu na kubaki single mother/father, wengine wanauana kabisa
 
Back
Top Bottom