Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaelewa unataka tuelewe nini...Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng
Sijaelewa unataka tuelewe nini...
Si kweli, mi sifahamu kiarabu lakini kiswahili nakifahamuIli Ujue Kiswahili Huna bud Kukifahamu KIARABU
Si kweli kisingekuwa kiarabu basi ingekopa maneno kutoka lugha nyingine
Hii ni sawa na kusema bila nyerere tusingepata uhuru
Babaticha, nikuulize maswali kwanza:
1. Umefanya utafiti gani au umetumia utafiti wa nani kudhihirisha jambo hilo?
2. Je, una takwimu gani juu ya jambo hilo?
3. Je, unaweza kututajia lugha hata moja tu ambayo haina maneno kutoka lugha nyingine?
Baada ya maswali hayo nikupe mawazo yangu. Hakuna lugha hata moja inayoishi bila kuchukua maneno kutoka lugha nyingine. Kichwa chako cha uzi huu ni cha kustaajabisha kwa namna mbaya.
Siku hizi mtandao unakupa habari haraka na kwa urahisi. Sasa hivi nimegoogle na kukuta asili ya maneno yafuatayo ambayo tunayajua kama ni ya Kiingereza: government,judge, parliament, attorney (French), physics, zoology, botany, drama, comedy (Greek), animal, exit, science (Latin), alcohol, algebra, zero, sugar (Arabic), nk. Kuna orodha ndefu tu. Je, tuseme kwamba Bila Kiarabu/Kifaransa/Kigiriki hakuna Kiingereza maana kuna maneno yametoka kwenye Kiarabu?
Mtaalamu mmoja wa Kiingereza aliyejulikana kama Robins alifanya utafiti miaka ya 60. Alitafuta maneno 10,000 yanayotumika sana katika Kiingereza. Kisha akatafuta vyanzo vya maneno hayo. Akagundua kwamba asilimia kama 37 tu ya maneno hayo yalitoka katika Kiingereza asilia. Mengine yalitoka kwenye Kifaransa, Kilatini, Kigiriki na lugha nyingine. Lugha hizi ziliingiza maneno katika Kiingereza baada ya kuwa tayari kuna Kiingereza. Naamini ni upuuzi kudai kwamba bila Kifaransa hakuna Kiingereza
Jitahidi kujenga hoja kwa mantiki na data jarabati.
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng
Mtoa mada anakisudia kuwa kiswahili kimeazima maneno mengi ya lugha ya kiarabu jinsi nlivyomuelewa mimi
kweli hakuna lugha ambayo haijakopa maneno katika lugha nyingine,hata kiarabu kimeazima maneno lugha nyingine
Mfano neno lemon ni kiingereza lakini warabu wanalitumia likiwa na maana ile ile,limao
Nataka nikuonyeshe umetumia maneno mangapi ya yanayotoka katika kiarabu happ juu,
1,kudhihirisha
2,lugha
3,maswali
4,asili
5,mtaalamu
6,sitini
7,asilia
Hayo ni baadhi tu yanayotoka kwenye kiarabu
Nadhani anamaanisha kwamba matamshi yanafanana,.Mfano kuna maneno ya kichina yanatamkwa saswsawa kama kiswahili au kiingereza ila ktk uandikaji ni tofautiHayo maneno mbona hayaandikwi kwa kutoka kulia kwenda kushoto?
Ili Ujue Kiswahili Huna bud Kukifahamu KIARABU
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng