Bila kiarabu hakuna kiswahili

Babaticha

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
26
Reaction score
1
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng
 
Sijaelewa unataka tuelewe nini...
 
Hayo maneno mbona hayaandikwi kwa kutoka kulia kwenda kushoto?
 
Si kweli kisingekuwa kiarabu basi ingekopa maneno kutoka lugha nyingine

Hii ni sawa na kusema bila nyerere tusingepata uhuru
 
Babaticha, nikuulize maswali kwanza:
1. Umefanya utafiti gani au umetumia utafiti wa nani kudhihirisha jambo hilo?
2. Je, una takwimu gani juu ya jambo hilo?
3. Je, unaweza kututajia lugha hata moja tu ambayo haina maneno kutoka lugha nyingine?
Baada ya maswali hayo nikupe mawazo yangu. Hakuna lugha hata moja inayoishi bila kuchukua maneno kutoka lugha nyingine. Kichwa chako cha uzi huu ni cha kustaajabisha kwa namna mbaya.
Siku hizi mtandao unakupa habari haraka na kwa urahisi. Sasa hivi nimegoogle na kukuta asili ya maneno yafuatayo ambayo tunayajua kama ni ya Kiingereza: government,judge, parliament, attorney (French), physics, zoology, botany, drama, comedy (Greek), animal, exit, science (Latin), alcohol, algebra, zero, sugar (Arabic), nk. Kuna orodha ndefu tu. Je, tuseme kwamba Bila Kiarabu/Kifaransa/Kigiriki hakuna Kiingereza maana kuna maneno yametoka kwenye Kiarabu?
Mtaalamu mmoja wa Kiingereza aliyejulikana kama Robins alifanya utafiti miaka ya 60. Alitafuta maneno 10,000 yanayotumika sana katika Kiingereza. Kisha akatafuta vyanzo vya maneno hayo. Akagundua kwamba asilimia kama 37 tu ya maneno hayo yalitoka katika Kiingereza asilia. Mengine yalitoka kwenye Kifaransa, Kilatini, Kigiriki na lugha nyingine. Lugha hizi ziliingiza maneno katika Kiingereza baada ya kuwa tayari kuna Kiingereza. Naamini ni upuuzi kudai kwamba bila Kifaransa hakuna Kiingereza
Jitahidi kujenga hoja kwa mantiki na data jarabati.
 
Ni sawa na kusema bila kilatini hakuna kiingereza. Tatizo lako wewe Babaticha haswa sasa ni lipi?
 
Last edited by a moderator:
Si kweli kisingekuwa kiarabu basi ingekopa maneno kutoka lugha nyingine

Hii ni sawa na kusema bila nyerere tusingepata uhuru

Mtoa mada anakisudia kuwa kiswahili kimeazima maneno mengi ya lugha ya kiarabu jinsi nlivyomuelewa mimi
 
kweli hakuna lugha ambayo haijakopa maneno katika lugha nyingine,hata kiarabu kimeazima maneno lugha nyingine
Mfano neno lemon ni kiingereza lakini warabu wanalitumia likiwa na maana ile ile,limao

Nataka nikuonyeshe umetumia maneno mangapi ya yanayotoka katika kiarabu happ juu,

1,kudhihirisha
2,lugha
3,maswali
4,asili
5,mtaalamu
6,sitini
7,asilia
Hayo ni baadhi tu yanayotoka kwenye kiarabu
 
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng

maneno haya nayo ni kiarabu?...kompyuta, barabara, meza, kung'atuka....?
 
Ninachokiona mimi ni kwamba ktk kiswahili tunasema kuna maneno mengi ya Kiarabu ni kwa sababu hatuna ufahamu wa lugha nyingine japokua hata hicho kiarabu hatukijui,zaidi ni kukariri vimaneno vichache:Lugha ya kiswahili tuko vibaya,kiarabu chenyewe ndo kabisa hatukijui,kiingereza ndo balaa,kichina ndo hata ndoto hatuoti;maisha yetu kama ya ndoto ndoto hivi,..Tutabishana hapa hadi tutaacha shughuli zetu za msingi na hakutakua na suluhu.Ukweli ni kwamba kila lugha imetohoa maneno kutoka kugha nyingine,na hiyo ni tabia ya kila lugha..

Ni kweli,mfano neno Lemon:
Kiingereza=Lemon Kichina =Lemon Kiswahili =Limao (ni kwa matamshi sio kuandika)

Neno Baba
Arabic=Baba Chinese=Baba Persian=Baba Greek=Baba Turkish=Baba Swahili=Baba Yoruba=Baba
Sasa sijui lugha ipi ilikopa kwa mwezie hapo.. (ni kwa matamshi sio kuandika)
 
Hayo maneno mbona hayaandikwi kwa kutoka kulia kwenda kushoto?
Nadhani anamaanisha kwamba matamshi yanafanana,.Mfano kuna maneno ya kichina yanatamkwa saswsawa kama kiswahili au kiingereza ila ktk uandikaji ni tofauti
 
Kiburi,dhulma kafiri,nafsi,zinaa,kaburi,mauti,laana,binadamu,shari na kadhalika haya yote yanatumika kiarabu na sisi waswahili na maana ni ile ile yan hadi kichwa kinauma.
 
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng

umeolewa na mwarabu, your love is your weakness, you need to see the forest before seeing the tree babe.
 
Hili linathibitika kwa Uwepo wa Idadi kubwa ya Manen ya Kiswahili amby yanatokana na Kiarabu tofaut na Lugha nyingine,Mfano:-
LAFUDHI,RADHA,FAHAMU,FALSAFA, JAMAA,BARIDI,SWAHILI, ABUDU.SAWIA,Na mengn meng

Kiswahili asili yake ni lugha za kibantu na si kweli kwamba bila kiaribu kusingekuwa na kiswahili.

Rejea utafiti wa watafiti wa lugha ya kiswahili, 65% lugha za kibantu, 35% kiarabu na 5% lugha zingine. Pia kumbuka lugha yoyote ina sifa ya kukopa maneno kutoka lugha nyingine hivyo kuwa na maneno ya kiarabu kwenye kiswahili si hoja yenye mashiko kuwa kiswahili ni kiarabu.
 
Mimi naona mtoa mada anajaribu kukikuza kiarabu na kuonyesha kuwa bila kiarabu kiswahili hakipo. Hii si kweli, hebu angalia katika usemi huu kuna neno lipi la kiarabu...

"wambe wao mie sambi
sambi nao si walumbi

sendi nao si wajuzi
mambo yao ni yakipuuzi"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…