Bila kujali una itikadi ya chama,je kuruhusu mauaji ni halali?

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Kiubinadamu,ni kosa kubwa na kinyume cha utawala wa kisheria na haki za binadamu kuruhusu mauaji ya raia wakaidi.Kwa mujibu katiba ya nchi ibara ya 6(b),(c) na (e),kutokana ibara hii Mh Pinda amevunja katiba aliyoapa kuilinda.Na kuna wachache ambao akili zao zimejaa tope wanaunga mkono kauli ya kichochezi ya Pinda,akiwemo mzee wa usingizi.
Najiuliza hivi hawa wangekuwa ndio ndugu zao wamekufa wangeshabikia kauli ya kipuuzi kama hii? Hakika nawambia siku yaja,hata siku ya mwisho hizi dhambi mnazozifanya satan atakuja kuzikataa.
Wanataka waripuliwe wake zao,watoto wao,mashemeji zao ndio wajue kuwa ni hatari? Siku atakakufa kiongozi mmojawapo wa ccm ndipo watajua kuwa ni hatari? Kila mtu ana haki ya kuishi kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara ya 12 kifungu kidogo cha 1 na 2,pia ibara ya 13 kifungu kidogo cha 1-4.
Sasa mh pinda anatoa wapi ujasiri huu wa kuropoka? Kavunja katiba,na kwa kuwa ndio mtendaji na msimamizi wa shughuli zote za serikali,hivyo basi kuua ni msimamo wa serikali na si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…