Wala wstanzania siyo Mbumbu, Rushwa pia siyo Tatizo, kwa sababu rushwa unaweza ukapokea na ukafanya yako, Vyombo vya dola wala havina makosa yoyote wanatimiza wajibu wao kutokana na mfumo wa sheria uliopo kwa sasa. Tatizo ni moja tu, katiba tu, huwezi ukashiriki uchaguzi wakati wasimamizi wote ni waajiriwa wa mwenyekiti wa chama mnachoshindana nacho, mimi ni washauri wapinzani wala wasitumie nguvu nyingi kudefend huu uchaguzi bali waweke nguvu nyingi kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Wakewekeza nguvu nyingi kwenye huu uchaguzi wakiini macho watakosa watu wakupigania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, mimi mwenyewe sitapiga kura tena kwa katiba hii na tume hii afadhali nijilie ugali wangu na maharage kuliko kufanywa mjinga na mimi nikubali. Afadhali ata uchaguzi wa chama kimojavunashamra shamra kuliko huu. Siamini kuwa hivi vitu vinatokea bahati mbaya la hasha hatahao tunao waweka mbele wala si waaminifu wananchi kama wananchi wenyewe wanatakiwa wachukue hatua, je ni njia gani, mimi sijui ila naamini hsta kama njia ni nyembamba na imesonga basi ndiyo hiyo hiyo tupite lasivyo tukubaliane na hali halisi, kwasabu miongozo ikishatolewa juu huku chini ni kutekeleza tu, tunaweza tukawaonea watendaji na wasimamizi wasaidizi lakini wao watafanya nini na ni waajiriwa waseikali wataacha kumtii bosi wao wamsikilize Mbowe na Tundulisi. Tunapaswa tupiganie Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi hata kama watu watapotezwa kama wakina Ali, kibao nawakina soka lakini mapambano yakiendelea watasurender tu