Bila Mshikamano wa Kitaifa, Tanzania tuitakayo itakuwa ndoto kuiona

Bila Mshikamano wa Kitaifa, Tanzania tuitakayo itakuwa ndoto kuiona

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,687
Reaction score
1,111
Bila mshikamano wa kweli Tanzania tuitakayo itakuwa ni sawa na ndoto za Alinacha.Tutaimba sana amani na umoja lakini haki bila wajibu au wajibu bila haki ndiyo silaha pekee ya kuvunja umoja wetu wa kitaifa ulioasisiwa na Mwalimu J K nyerere.

Watawala wamepata mashaka juu ya kuvunjika kwa umoja wetu wa kitaifa,lakini wakashindwa kutambua kila mbegu bora uipandayo na kuimwagilia vizuri lazima itamea juu ya ardhi.Mbegu iliyopandwa na kumwagia vizuri ya ukabila,udini na ukanda ilikuwa kama wimbo wa taifa katika kipindi cha uchaguzi kwa kuwagawa na kusahau misingi bora ya utaifa iliyosimikwa na viongozi wetu wa awali.

Mshikamano huu leo hii unazidi kushika kasi ya kuvunjika kutokana na kudharauliana na kupuuzana katika ya mtu mmoja hadi mtu mwingine.Kupuuzana huko ndiko kulikopelekea watawala wetu kutunyang'anya ardhi na kuwapa wageni kwa bei sawa na bure. Mshikamano huu uliovunjika ndiyo uliopelekea watawala kutothamini umoja wetu wa kitaifa na kuamau kufisidi mali za umma kwa maslahi ya wachache na familia zao.

Serikali moja inatoa kauli pingamizi mbili kama vile hawakai pamoja na kuamua mambo yao pamoja.Leo utasikia rais ana sema hivi baadae kidogo kauli ile ile itapingwa na waziri mkuu ambao wote ni wa serikali ya chama kimoja. Serikali hiyo hiyo ndiyo yenye kuruhusu ndege za kijeshi za taifa jingine kupitia ikulu kutua ndani ya anga la Tanzania na kuchukua wanyama wetu bila kufuata taratibu na serikali hiyo hiyo kujifanya kipofu juu ya sinto fahamu ya sakata hilo.

Wananchi wamepoteza mshikamano kiasi cha kuamua kurubuniwa na kuuza haki yao ya kuchagua viongozi wawatakao kwa kuuza vipande vyao vya kupigia kura na kukosa ile haki ya kikatiba ya kumchagua wamtakaye.

Umoja wetu ambao tuliishi kijamaa bila kujali itikadi zetu leo umebadilika na udini kuchukua nafasi yake. Mapigano ya kikabila nayo yameshika kasi,wafugaji na wakulima wana nyukana,Watanzania wanaitwa wavamizi katika ardhi yao ilihali wageni wakipewa hifadhi na kulindwa kama miungu watu ndani ya taifa linalo amini kuwa ni nchi ya amani.

Wageni toka China wakiendelea kuwashambulia raia wetu na kupewa kinga na vyombo vyetu vya dola kwa kuwa tu wamepewa mlungula ama kishika tumbo. Kuvunjika kwa mshikamano na umoja wa kitaifa umesababisha maadili ya jamii kupotea na taifa kuingia katika mfumo wa kimagharibi na kuwakumbatia wa magharibi na kusahau mila na desturi za kitanzania.

Tusipokuwa kuwa wakweli kwa kufumbiana macho na kuendekeza tabia ya kulindana itasababisha hali ya amani ndani ya nchi yetu kupotea kabisa kwa kujenga chuki miongoni mwetu.

Ni bora tutafute njia muafaka wa kutatua matatizo yetu yanayo sababisha mshikamano huu na umoja wa kitaifa kupotea,tafakari!!!!
 
Katika miaka ya 1980 ya chama kimoja licha ya changamoto zilizokuwepo, nchi hii ikiongozwa na CCM bado kulikuwa na walau asilimia fulani ya mshikamano wa watanzania. Mwl Nyerere katika eneo hili alisimamia sana utu wa watanzania na kujaribu kujenga uzalendo. Mafunzo ya shule na JKT yaliwaweka watanzania katika mizania moja na kwa kiasi fulani watanzania walikuwa wanapendana.

Kuja kwa vyama vingi na kuondoka kwa azimio la Arusha kunatajwa kuwa sababu za kudhoofika kwa mshikamano wa kitaifa. Kuondoka kwa azimio la Arusha kulifunguwa fursa ya wenye uwezo kutawala uchumi na siasa za nchi na kufanya matabaka katika jamii.

Vyama vingi navyo vimeibuwa sakata la kuporomoka kwa mshikamano wa kitaifa. Hapa CCM inatajwa kushindwa kuweka misingi ya kulinda mshikamano. Vyama vingi viliruhusu USHINDANI WA SERA na UTAWALA WA NCHI. Vyama vimeibuwa uhasama wa kiitikadi na kupelekea mmomonyoko wa mshikamano. Kwa mfano usipokuwa CCM hata kama una kipawa huwezi kupata fursa muhimu ya kimaamuzi kutokana na kuwa na tofauti ya kiitikadi. Hali hii imepelekea nchi kuegemea katika milengo ya kisiasa tu na kuacha matumizi ya vipawa katika kuijenga nchi.

CCM inalaumiwa tena kutoweka maandalizi ya kimfumo ili uendane na mabadiliko ya vyama vingi. Leo hii Rais anateuwa wale anaowaamini kuwa makada wa CCM na hata suala la ajira kwa vijana linahusishwa na itikadi. Vile vile fursa za uwekezaji na biashara nyeti na hata mikataba minono nayo inahusishwa na uchama.

Kwa awamu tatu za vyama vingi (awamu ya 3,4 na 5)bado CCM imetumia fursa ya ubovu wa Katiba yetu kulipotezea suala la mshikamano wa kitaifa katika mazingira ya vyama vingi ambapo chama kinachoshinda kinabeba utawala wote. CCM imekuwa mshindi kwa awamu zote na haijalitendea vyema Taifa suala hili nyeti.

Ushindani wa vyama unaipa fursa CCM kutumia vyombo vya Dola, Sheria, Mahakama na hata Bunge kupitisha na kulinda maslahi yake. Ukuu wa mamlaka ya Rais kuteuwa na kupanguwa unatumika vyema na Watawala wa CCM kudhoofisha mshikamano wa kitaifa.

Kwa mtazamo wangu Tanzania kama taifa wakati umefika sasa wa kujadili hii hali na kuweka mambo sawa.

Hali iliyopo ya kudhoofika kwa mshikamano wa kitaifa kunachangiwa na KATIBA yetu kutoendana na matakwa ya wakati ambapo mshindi ndiye mwenye maamuzi hali ambayo CCM imeitumia kulinda maslahi yake.

HATARI ILIOPO MBELE.

Kuna hatari siku moja kukazuka mapambano ya ukabila ambapo kabila fulani litajikuta kuwa wanaunga mkono chama fulani na kushindwa kushirikishwa katika uendeshaji wa nchi kutokana na itikadi. Hali hii kwa mtazamo wangu inakuwa kwa kasi sana.Sambamba na dini tofauti, maeneo wanayotoka watu na hata rika.Viashiria kwa sasa sio vizuri.

Kukuwa kwa matabaka ya walionacho na wasionacho kutokana na fursa za kiuchumi kuhodhiwa na watu wanaotokana na watawala.

SOMO KUTOKA ZANZIBAR.

Tokea kuja kwa vyama vingi hali hii imeelezwa kuathiri sana Zanzibar. Kuna taarifa watu kutoka Pemba katika SMZ kubaguliwa na kufukuzwa, Wapemba wamekuwa wahanga wa hali hii eti kwa sababu wengi wao ni wapinzani. Katika hali hio, hata wale wapemba ambao ni CCM hawaaminiki.

Tatizo ni kukosa maandalizi na CCM iko kimya hadi sasa kushindwa kubadilisha na kurekebisha (accomodate) siasa yetu na mshikamano wetu.

Tanzania ya Mshikamano inawezekana.

Kishada.
 
Katika miaka ya 1980 ya chama kimoja licha ya changamoto zilizokuwepo, nchi hii ikiongozwa na CCM bado kulikuwa na walau asilimia fulani ya mshikamano wa watanzania. Mwl Nyerere katika eneo hili alisimamia sana utu wa watanzania na kujaribu kujenga uzalendo. Mafunzo ya shule na JKT yaliwaweka watanzania katika mizania moja na kwa kiasi fulani watanzania walikuwa wanapendana.

Kuja kwa vyama vingi na kuondoka kwa azimio la Arusha kunatajwa kuwa sababu za kudhoofika kwa mshikamano wa kitaifa. Kuondoka kwa azimio la Arusha kulifunguwa fursa ya wenye uwezo kutawala uchumi na siasa za nchi na kufanya matabaka katika jamii.

Vyama vingi navyo vimeibuwa sakata la kuporomoka kwa mshikamano wa kitaifa. Hapa CCM inatajwa kusahindwa kuweka misingi ya kulinda mshikamano. Vyama vingi viliruhusu USHINDANI WA SERA na UTAWALA WA NCHI. Vyama vimeibuwa uhasama wa kiitikadi na kupelekea mmonyoko wa mshikamano. Kwa mfano usipokuwa CCM hata kama una kipawa huwezi kupata fursa muhimu ya kimaamuzi kutokana na kuwa tofauti ya kiitikadi. Hali hii imepelekea nchi kuegemea katika milengo ya kisiasa tu na kuaha matumizi ya vipawa katika kuijenga nchi.

CCM inalaumiwa tena kutoweka maandalizi ya kimfumo ili uendane na mabadiliko ya vyama vingi. Leo hii Rais anateuwa wale anaowaamini kuwa makada wa CCM na hata suala la ajira kwa vijana linahusishwa na itikadi. Vile vile fursa za uwekezaji na biashara nyeti na hata mikataba minono nayo inahusishwa na uchama.

Kwa awamu tatu za vyama vingi (awamu ya 3,4 na 5)bado CCM imetumia fursa ya ubovu wa Katiba yetu kulipotezea suala la mshikamano wa kitaifa katika mazingira ya vyama vingi ambapo chama kinachoshinda kinabeba utawala wote. CCM imekuwa mshindi kwa awamu zote na haijalitendea vyema Taifa suala hili nyeti.

Ushindani wa vyama unaipa fursa CCM kutumia vyombo vya Dola, Sheria, Mahakama na hata Bunge kupitisha na kulinda maslahi yake. Ukuu wa mamlaka ya Rais kuteuwa na kupanguwa unatumika vyema na Watawala wa CCM kudhoofisha mshikamano wa kitaifa.

Kwa mtazamo wangu Tanzania kama taifa wakati umefika sasa wa kujadili hii hali na kuweka mambo sawa.

Hali iliyopo ya kudhoofika kwa mshikamano wa kitaifa kunachangiwa na KATIBA yetu kutoendana na matakwa ya wakati ambapo mshindi ndiye mwenye maamuzi hali ambayo CCM imeitumia kulinda maslahi yake.

HATARI ILIOPO MBELE.

kuna hatari siku moja kukazuka ukabila ambapo kabila fulani litajikuta kuwa wanaunga mkono chama fulani na kushindwa kushirikishwa katika uendeshaji wa nchi kutokana na itikadi. Hali hii kwa mtazamo wangu inackuwa kwa kasi sana.Sambamba na dini tofauti, maeneo na hata rika.Viashiria kwa sasa sio vizuri.

Kukuwa kwa matabaka ya walionacho na wasionacho kutokana na fursa za kiuchumiu kuhodhiwa na watu wanaotokana na watawala.

SOMO KUTOKA ZANZIBAR.

Tokea kuja kwa vyama vingi hali hii imeelezwa kuathiri sana Zanzibar. Kuna taarifa watu kutoka Pemba katika SMZ kubaguliwa na kufukuzwa, Wapemba wamekuwa wahanga wa hali hii eti kwa sababu wengi wao ni wapinzani. Katika hali hio, hata wale wapemba ambao ni CCM hawaaminiki.

Tatizo ni kukosa maandalizi na CCM iko kimya hadi sasa kubadilisha na kurekebisha (accomodate) siasa yetu na mshikamano wetu.

Tanzania ya Mshikamano inawezekana.

Kishada.
uko sahihi, ccm ni wakoloni weusi
 
Sisi wananchi tulitoa maoni ya kubakia na Chama kimoja....Kwa maoni yako CCM itekeleze maoni ya wananchi na kurejesha mfumo wa Chama kimoja?
 
Huwezi kuwa na mshikamano kwenye nchi inayoongozwa na nduli na dikteta uchwara mwenye roho mbaya kuliko hata shetani aliyejawa chuki za kutisha na visasi vya kila aina. Kauli zake ni vitisho tu chuki na dharau za hali ya juu kwa kujiona yeye ni kama mungu mtu. Tuna janga kubwa sana la Taifa la kuongozwa na huyu aliyekataliwa kufanyiwa kampeni na hata na mkewe.
 
Katiba mpya ni muhimu sana kwa umoja wa kitaifa bila katiba mpya Tanzania haitakuwa taifa tunalolifikiria. Jirani zetu Kenya baada ya machafuko ya 2007 walipata katiba mpya na leo tunaona hatua kubwa waliopiga katika masuala mengi.
 
Sisi wananchi tulitoa maoni ya kubakia na Chama kimoja....Kwa maoni yako CCM itekeleze maoni ya wananchi na kurejesha mfumo wa Chama kimoja?

Hapana.

Irekebishe KATIBA iendane na matakwa ya sasa ya kidemokrasia na kulinda mshikamano wetu.
 
Katiba mpya ni muhimu sana kwa umoja wa kitaifa bila katiba mpya Tanzania haitakuwa taifa tunalolifikiria. Jirani zetu Kenya baada ya machafuko ya 2007 walipata katiba mpya na leo tunaona hatua kubwa waliopiga katika masuala mengi.

JK alitaka kujaribu hili la walau kuthubutu kuchokoza maoni ya watanzania. Lakini alifeli kutokana na CCM
 
Huwezi kuwa na mshikamano kwenye nchi inayoongozwa na nduli na dikteta uchwara mwenye roho mbaya kuliko hata shetani aliyejawa chuki za kutisha na visasi vya kila aina. Kauli zake ni vitisho tu chuki na dharau za hali ya juu kwa kujiona yeye ni kama mungu mtu. Tuna janga kubwa sana la Taifa la kuongozwa na huyu aliyekataliwa kufanyiwa kampeni na hata na mkewe.
Semea nafsi yako cc tuko na Rais wetu mpendwa here job only!!
 
Alaumiwe nani saa? viashiria vinazidi kila kukicha au tunasubiri mpaka watu wauwane?
 
Katiba mpya ni muhimu sana kwa umoja wa kitaifa bila katiba mpya Tanzania haitakuwa taifa tunalolifikiria. Jirani zetu Kenya baada ya machafuko ya 2007 walipata katiba mpya na leo tunaona hatua kubwa waliopiga katika masuala mengi.

Hili watawala wa CCm hawataki kulisikia. UBOVU wa katiba yetu ndio chaka lao la kuingilia madarakani na kunufaika na rasilimali za nchi yetu wao na watoto wao.
 
kuna jamaa aliniambia kwamba,Panzi anaporuka uwa ameshaweka uwelekeo wa wapi atakwenda kutua hata kama kutatokea kitu kikae njiani itabidi ajigonge kwenye hicho kitu maana awezi kubadili njia akisharuka na ndio maana mtu akikuambia kwamba,una akili kama Panzi uwa ni tusi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom