Louis II
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 3,030
- 4,647
Huu mwaka umeanza kutujia vizuri kabisa na tunaanza kuyaona matunda ya juhudi zetu za "miaka nenda rudi" katika kujiinua kisoka.
Ni ukweli usiopingika, tumekuwa watazamaji kwa wenzetu kwa miaka mingi sana (japo mwaka 2009 tulibahatika kushiriki CHAN japo hatukufanya vizuri sana) ila nina imani Mwaka huu ni wa neema kwa Sisi Watanzania kisoka.
Ipo hivi,
KWANZA: Tumepata bahati ya kuandaa mashindano ya AFCON (U-17) yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao (April) na kushirikisha nchi nane (8). Mashindano haya yatasaidia kutangaza soka letu (hasa la vijana) kimataifa na bila shaka maskauti wa Soka kutoka vilabu tofauti watakuwepo na vijana wetu watapata nafasi ya kuonekana na hatimaye kupata soko nje ya nchi Kusakata kabumbu.
PILI: Klabu ya soka ya Simba imetutoa kimasomaso Watanzania baada ya kutinga hatua ya robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Africa (CAFCL#2018/19) haya ni mafanikio makubwa sana kwetu Watanzania hasa ukizingatia kuwa vilabu vyetu vimefurukuta kwa miaka mingi kufikia hatua hii ila vimeshindwa. Japo wengi wetu tunachukulia "simple" but hii ni platform kwa vilabu vyetu kujengeka katika saikolojia ya "ushindi na mafanikio" bila kukata tamaa. Hongereni Simba, Watanzania tumefurahi na tunajivunia mafanikio yenu.
TATU: Timu yetu ya taifa "Taifa Stars" Jumapili hii ya tarehe 24/03/2019 inaenda kuandika historia mpya mbele ya Uganda "Cranes". Iwapo Taifa Stars itashinda mechi hiyo huku ikiiombea mabaya timu ya Lesotho dhidi ya Cabo Verdè, basi timu yetu itakuwa imefuzu kucheza AFCON 2019 Nchini Egypt. Uwezekano wa Taifa Stars Kushinda ni mkubwa kwa wachezaji wana ari na matumaini makubwa ya kuwaduwaza Waganda pale "Kwa Mkapa" Lakini pia hamasa ni kubwa sana kwa Watanzania ambao wana matumaini kwa timu yetu kufanya vizuri na hatimaye kufuzu AFCON tangu tulipofanya hivyo miaka 39 iliyopita yaani 1980 nchini Nigeria.
Mungu ibariki "Taifa Stars", Ibariki "Serengeti boys", Ibariki "Simba Sports Club", Ibariki Tanzania.
#2019NiMwakaWetu
#TanzaniaFirst
#TanzaniaForTanzanians.
#Amen