Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 677
BILA VITU,MTU ANAKUWAJE NA MAENDELEO!?
Leo 11:30hrs 11/10/2020
Utajiri wa mtu unatokana na vitu alivyonavyo,vivyo hivyo Utajiri wa Taifa unatokana na pato la taifa linalotokana na vitu kama miundo mbinu ya bandari,miundo mbinu ya barabara,miundo mbinu ya reli ya kisasa ya Umeme,miundo mbinu ya ndege na viwanja vyake,miundo mbinu ya Umeme mfano wa Bwawa kubwa la Umeme la Mwalimu Nyerere,Wilayani Rufiji,na Maendeleo ya teknolojia,kwa ujumla,haya ni mawasiliano yanayorahisisha Maendeleo ya binadamu katika nyanja zote,
Kwa pamoja vitu hivi vyoote vitachagiza Ujenzi wa Viwanda utakaotumia malighafi za kilimo chetu,hivyo Wakulima watafaidika,bidhaa zitakazozalishwa viwandani zitaleta biashara ambayo itaingiza kodi kwa taifa,Sasa kupata thamani na utajiri wa Taifa la Tanzania,tunachukua pato la taifa linalopatikana toka kwenye biashara na miundo mbinu yote tunagawa na idadi yetu wote sisi Watanzania,tunapata thamani ya hela ambayo imelipeleka Taifa la Tanzania kwenye Uchumi wa kati,
Maendeleo ya vitu ni muhimu sana kupima uthamani wako,lakini kupanga ni kuchagua,mtu mwingine kula chipsi kuku ndio kipaumbele chake,mwingine bia nyama choma ndio kipaumbele chake,wakati mwingine ili aishi lazima ajibane ajenge nyumba akae kwake,mwingine lazima ajibane anunue Range Rover au x5,kwa hiyo kupanga ni kuchagua,je ni vitu au wewe mwenyewe,kwa uwiano huo unaweza sasa kusema labda Maendeleo ya vitu si lengo la mwisho bali ni lengo litakalosaidia kupata maendeleo ya watu mfano ajira, kipato na mwishowe mahitaji ya kibinadamu kama dawa mahospitalini,Ujenzi wa dispensary na vituo vya afya,
Hapo nyuma ilipata kusemwa kuwa Ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora ni muhimu sana kwenye kufikia Maendeleo,lakini Mimi binafsi nina mashaka na siasa safi na Uongozi bora kama hivi vitu vimetusaidia sana,Tumekuwa na shida ya pseudo-politics na pseudo-leaders ambavyo vimekuwa vinajitafutia na kujitafuta bila kujali maslahi mapana ya watu,kwa hiyo binafsi Mimi ni mdau wa Maendeleo ya vitu hata sasa ninatamani kujenga ghorofa na kununua pira,sio gari bali pira la hatari kama v8 hivi,hii kwangu ndio Maendeleo.
-Scale of Preference.
(Maendeleo ya vitu).
Watu wataendelea kukiwa na maendeleo ya vitu,siku zote maendeleo ya watu yataletwa kukiwa na mazingira wezeshi ya watu hao mfano Teknolojia, miundombinu ya barabara, Umeme, amani,ndio huleta maendelo ya watu,kumbuka tu kwamba haviwezi kuja vyote kwa pamoja. Tumejidanganya zaidi ya Miaka 50 kuleta vyote pamoja tumefeli. Lazima maendeleo ya vitu yatangulie ndipo maendeleo ya watu yafuate,kupata maendeleo ya watu kabla maendeleo ya vitu hayajatengamaa vizuri yaani maendeleo ya vitu ndo yanapelekea maendeleo ya watu lakini kinyume chake siyo sahii, in english!
Economic growth(maendeleo ya vitu) ndio yanapelekea economic development( maendeleo ya watu)
If you can not achieve qualitative and quantitaive developments if quantitative development is poor ingawa maendeleo ya vitu yanaweza pia yasilete tija katika maendeleo ya watu kama maendeleo ya vitu yatafanywa na machines or robots au automation systems lakini mwisho wa siku barabara lijengwe na mashine au riboti baada ya hapo itatumiwa na binadamu,daraja lijengwe na roboti au mashine bado litatumiwa na binadamu,
Maendeleo ya watu ya kula pasipo kupanda,kuvuna usichopanda,ama Maendeleo rahisi ya kuvuna bila kupanda,nikiwa na maana kuwa yafanyike mambo ambayo manufaa yake yanakuja papo kwa hapo,basi yawezekana taifa hili likabaki kuwa taifa changa kiuchumi kwa zaidi ya miaka 500 ijayo,Vitu avifanyavyo Rais John Magufuli hivi sasa vitachagiza sana shughuli za maendeleo, hivyo kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi,toka tupate uhuru hadi kufikia leo hii tuna zaidi ya miaka 50 na bado hatujafikia katika uchumi wa kujitegemea, hivyo nadhani jitihada zinazo fanyika katika kuboresha uchumi wa taifa zinaweza kutusogeza japo kwa kiasi fulani kufikia Miaka mitano au kumi ijayo,
Pia tusisahau ya kuwa hakuna taifa lililo endelea pasipo kizazi fulani au cha kipindi fulani kuvuja jasho,hata kwa mtu binafsi pia lazima avuje jasho ili kupata maendeleo,lazima ulimie juani kisha ulie kivulini,hakuna njia ya mkato wala maghumashi,nimalizie kwa kusema,Uchumi wa watu unakuja baada ya uchumi wa vitu ila tusitegemee tutoke jasho siku moja ununue gari au ujenge nyumba! Inahitaji uvumilivu kwa maana inachuku miezi hata Miaka,
Rais John Pombe Magufuli amejenga miundo mbinu ya ndege na kununua ndege,hivi leo watalii wameongezeka kwa kupanda ndege zetu za moja kwa moja toka katika nchi zao na pato la taifa limeongezeka,tumeona Tanapa wakitoa gawio kwa Serikali,sio tu gawio bali gawio la bilioni 650,hii ni faida kubwa kiuchumi baada ya Ununuzi wa ndege kubwa kumi,dreamliner,Airbus na Bomberdier,Rais John Pombe Magufuli amejenga vituo vipya vya afya 400 ikiwapo kituo cha Afya cha Kalya ambacho kilimpatia matibabu ya awali Ndugu Zitto Kabwe baada ya kupata ajali njiani akiwa safarini,haya ni matunda ya Maendeleo ya vitu kwa kujengwa vituo vya afya nchi nzima,
Tatizo watu wanaolalamika oh kwa nini Rais Magufuli kawekeza kwenye Maendeleo ya vitu,watu awa hawana subira na walizoea maisha ya kuneemeka kijanja janja huku wengine wakitaabika hata kusomesha watoto ama kuwapa matibabu wanapohitaji,niseme tu Rais John Pombe Magufuli yuko sahihi katika uwekezaji tunaofanya,tunapaswa kujitahidi kusimama wenyewe bila misaada ya wazungu. Nchi inaendelea kirahisi ikiwa na miundo msingi yakutosha! Tupo vizuri.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854.
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.
-Research; Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.