Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BILALI REHANI WAIKELA (1932 – 2022)
Maneno hayo hapo chini yapo katika utangulizi wa kitabu cha Abdul Sykes:
‘’Napenda kutoa shukrani maalum kwa Bilal Rehani Waikela, muungwana wa Kimanyema na Muislamu wa kweli.
Waikela akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 1955, alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU mjini Tabora.
Waikela alinieleza jinsi Waislam kwa umoja wao walivyomuunga mkono Julius Nyerere na harakati za uhuru.
Vilevile alinieleza kwa muhtasari siku zake kizuizini pamoja na babu yangu katika gereza la Uyui, Tabora mwaka wa 1964 kwa kile kilichoitwa kosa la ‘’kuchanganya dini na siasa.’’
Nina deni kubwa kwake kwa kunipa picha za wakati ule na nyaraka zake binafsi juu ya ‘’mgogoro,’’ wa EAMWS uliozushwa mara baada ya uhuru.
Natoa shukrani kwa Waikela kwa kunitia hima na kunipa moyo kuandika kitabu ili nieleze historia ya kweli ya kuundwa kwa TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika na chamgamoto zilizozuka mara tu baada ya uhuru kupatikana.
Waikela tofauti na watu wengine waliozungumza na mimi aliniruhusu pia kumnukuu kwa jina bila ya uoga wowote katika mambo mazito yaliyotokea nchini ambayo wengi waliona uzito kuyaeleza lau kama wao wenyewe waliathirika na kuhusika moja kwa moja.
Alifurahi kuona kwamba historia ya kweli ilikuwa inaandikwa na habari alizonieleza zitakuja kutumika katika kuhifadhi historia ya nchi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Vilevile Waikela alinikutanisha na wazalendo wengine kama Mohamed Mangiringi, marehemu Ramadhani Singo na wengineo ambao nilizungumzanao kwa kirefu katika utafiti wangu.’’
(1998)

22