Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
RISALA YA EAMWS KWA RAIS NYERERE ILOYOSOMWA NA BILAL REHANI WAIKELA UKUMBI WA SHULE YA WASICHANA YA AGA KHAN 1963
''Siku kabla ya mkutano wa EAMWS mwaka wa 1963, Nyerere aliwaalika wajumbe wa mkutano Government House kwa chakula cha usiku.
Hao waalikwa walikuwa wajumbe waliochaguliwa mahsusi.
Waikela hakuwa mmoja wa hao waalikwa. Nyerere alichukua nafasi ile kuwashauri wajumbe wale waanzishe jumuiya ya Waislam wa Tanganyika ichukue nafasi ya EAMWS.
Wajumbe hawa walipoleta katika mkutano hoja ya kuanzisha jumuiya ya Waislam wa Tanganyika, Waikela alisimama na kuipinga hoja ile.
Alizungumza vilevile kuhusu uadui wa serikali kwa Waislam na Uislam.
Waikela alimaliza hotuba yake kwa kutoa changamoto kwa wajumbe wamuite Nyerere kwenye kufunga mkutano ili aje awaeleze wajumbe msimamo wake kuhusu kadhia hii ya chinichini baina ya serikali na Waislam.
Baada ya kushindwa kwa hoja ya kuivunja EAMWS wajumbe wa mkutano wakaona kuwa ingekuwa vyema Nyerere aitwe kufunga mkutano ule na asomewe makubaliano yaliyofikiwa.
Nyerere alifika kufunga ule mkutano na akakutana uso kwa uso na Waikela, ambae alimsomea maazimio ya mkutano.
Waikela alimfahamisha Nyerere kuwa umoja kwa Waislam ni fardh, ni wajibu wa lazima.
Ni kwenda kinyume na maamrisho ya Allah kuwagawa watu.
Baada ya utangulizi huu Waikela huku akimnyooshea Nyerere kidole alieleza uadui unaoonyeshwa na serikali dhidi ya Waislam.
Waikela alimaliza hotuba yake kwa kitisho.
Alimwambia Nyerere ikiwa Waislam watamgeuka kupambanana yeye hatakuwa na uwezo wa kuwashinda.
Nyerere alitulia tuli pembeni mwa Rais wa Baraza la Tanganyika la EAMWS Tewa Said Tewa akimsikiliza Waikela.
Aliposimama kujibu hotuba ya Waikela Nyerere kwa upole alisisitiza msimamo wa serikali wa kutoa haki na usawa kwa raia wake wote.
Kwa kiasi fulani Nyerere alikuwa amefanikiwa kupunguza joto kati ya Waislam na serikali.
Hotuba ya Waikela na ya Nyerere zikapewa umuhimu mkubwa katika radio.
Waislam wengi wakajitokeza stesheni ya gari moshi Tabora kuja kumpokea shujaa Waikela.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998)
Masahihisho si RTD bali TBC.