Bilion 20 Alizowekeza Mo Dewji Hazipo Popote Kwa Sababu Zimeisha Rasmi Msimu 2021/22

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Huyu mwana ni mjanja sana.

Yaani amejimilikisha Klabu kijanja janja tu (Kama asemavyo KIGWANGALAH)

Kwa namna anavyopenda kusifiwa na kupigiwa magoti nimeshangaa sana kuona kwanini haonyeshi hizo pesa mahala zilipo. Kama ni kweli benki kwanini asiseme ziko benki gani?

Kumbe uhalisia jamaa alikuwa anatoa bilion 4 kila msimu kwa mida wa misimu 5

Msimu 2021/22 - Yanga Bingwa
Msimu 2020/21 - Simba Bingwa
Msimu 2019/20 - Simba Bingwa
Msimu 2018/19 - Simba Bingwa
Msimu 2017/18 - Simba Bingwa

Kati ya hiyo misimu 5. Misimu 4 alifanikiwa kuchukua Ubingwa na msimu wa mwisho alifanikiwa kuchukua Bingwa wa kihistoria kwa sababu.

Yanga SC alifanikiwa kuchukua msimu huu kwa sababu ya pesa ya mkataba na Azam TV ambapo kila mwanzo wa msimu anapokea Bilion 4 sawa na kiasi ambacho Mo anakiwekeza Simba SC.

Ikumbukwe Azam TV ikakuwa ikitoa bilion 4 kila mwaka kwa mda wa miaka 10.
(Huenda ikawa sababu ya kwanini viongozi wa Yanga wanasema watatwaa ubingwa kwa mara 10 mfululizo)

Je nini hatma ya Mo Dewji pale Simba SC ikiwa ana miliki asilimia 49 ya hisa za klabu ikiwa pesa ajazikabidhi kwa klabu bali alikuwa anazikabidhi kwa kabla kwa mfumo wa kuihudumia timu?

Je nini kitatokea kwa simba kama mwana akisusa na kudai arudishiwe pesa zake?
 
Mo Dewji akihojiwa na Salama, alisema bilioni 20 atakazowekeza Simba atazipeleka benki, riba inayopatikana ndio itaendesha klabu, imekuwaje tena kaendesha klabu kwa kula mtaji? Na ni mfanyabiashara na anaijua Simba meaning alikuwa anajua anachoongea kwa uzoefu.
 

Alihojiwa lini?

Na alisema lini ataziweka?

Na kama alikuwa tayari kusema ataziweka benki, kwanini akiulizwa anakuwa mkali?

Wahindi sio wa kuwaamini sana. Kama Alisema Kambi ya simba msimu huu itakuwa Marekani na mwisho wa siku akawapeleka Ismailia kwenye mashamba ya miwa, kuna walakini.
 
we jamaa unatema madini sana ona sasa kawapeleka kwenye miwa ismailia, achana nao wajinga hawajastuka tu..vyanzo vyako ndani ya simba havijakuambia kuhusu hizo billions 20?
 
Mkalipe deni Uturuki hamna mkopo kule wala kulipa kidogokidogo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pesa za Magodoro fake zimekombwa zotee.
 
Uyo bwana tokea anaanza kupiga promo ya kutaka apewe simba tiyali waliosoma cuba tulikuwa tushanusa viashiria fulani fulani vya aya yanayotokea sasa, katiba ya simba ndo inayowanyonga kwa sasa, Unapokuwa na mwekezaji mmoja tena mwenye kupenda kusujudiwa na sifa lazima mpitie kwenye magumashi kama aya, mchakato wa Mo kupewa timu uliendeshwa kijanjajanja sana, na ulipelekwa haraka haraka baada ya kuwa amewaweka sawa wale alioona wanaweza kumkwamisha asipate anachokitaka kwa haraka, Maana aliona akichelewa hawa watu wataamka na kuhoji sana mchakato husika, ndo maana ukiongelea suala la transfomation yanga keshawapiga simba gape kubwa sana kwenye mchakato wao, Mchakato umeendeshwa kwa uwazi na katiba ya yanga iko vizuri sana, wawekezaji wanatakiwa zaidi ya mmoja na wasizidi 4, kwa maana iyo akuna kumlamba miguu mwekezaji Kama ajatimiza majukumu yake anakaa pembeni wenzake wanasonga mbele, Leo hii mchakato wa simba aueleweki umefikia wapi,,timu bado inaendeshwa kienyeji kienyeji mpaka wajumbe wa bodi wanaanza kukosa uvumilivu na kutoka hadharani kuongea namna wasivyofurahishwa na mambo yanavyoendeshwa, Mwisho wa siku uyu bwana naona kabisa anatafuta pa kutokea kwakuwa tiyali ashapata alichokuwa anakitafuta kwenye biashara zake
 
Wewe bhana acha kutuvuruga hapa! Mashabiki wa simba kwa umoja wetu tunataka mwekezaji aweke bilioni 20 mezani! Ikiwezekana tugawane mashabiki pamoja na wachezaji. Tulimtuma lini kwenda kuziweka benki hizo bilioni zetu 20?

Tumechoka kuitwa mbumbumbu na Makolo kwa sababu tu ya kumtetea mwekezaji janja janja. Nakuhakikishia asipotoa hizi bilioni 20 zetu msimu huu mpya wa ligi, aisee tutaandamana mpaka ofisini kwake.
 
Jezi elfu 30 yanga inapata 1300 badala muongelee ya kwenu mjikomboe unaongelea ya simba kumbe ndo maana mnaenda airport kuwapokea wageni wakija kucheza na simba kwasababu akili ni empty set mpaka mkambeba engineer hersi.
 

 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…