Bilionea Mengi atoa darasa kwa Muhongo

Hao wawekezaji anaowataka muhongo wanakuja kukopa kwenye bank zetu za ndani...
...na hapo ndipo wanaponiacha hoi, umenikumbusha ishu ya NBC iliuzwa kwa bilion 10 kama sikosei, jamaa wakaichukua wakauza nyumba zoote za benki wakapata hizo bilioni 10 wakailipa serikali wakachukua benki yao mpaka leo wanakula faida...
 

1. Nakubaliana na wewe tumepoteza fedha nyingi katika madini. lakini tulipoteza kwa sababu hatukujipanga katika service industry, vitu kama vyakula, ulinzi n.k vingeweza kushusha asilimia ya faida nzima (kama hiyo 97% uliyoweka) iliyokwenda nje. sasa huu ndio wakati wa kujipanga katika sekta ya gesi ili kuhakikisha mwekezaji analeta fedha tu, vingine vyote tunasupply wenyewe. Lakini ninachokupinga ni katika umiliki wa vitalu.

2. Elewa kwamba vitalu ni mali ya watanzania wote (zaidi ya milioni 40), ambao wengi ni maskini wa kutupwa. Ukirudia maelezo yako mwenyewe hapo juu, tayari umeshakubaliana na Prof Muhongo kuwa kina Mengi hawana pesa ya kuwekeza, ndio maana wanataka hilo unaloita "kapu maalum la wazawa". Kitu ambacho watakifanya ni kwenda kukopa mitaji kwa kutumia hizo licences kama collateral.
Sasa tatizo ni kuwa hakuna njia yoyote ambayo itahakikisha wote sisi wazawa (watu zaidi ya mil 40 ), tuna fursa/nafasi ile ile ya kupata leseni kama kina bwana Mengi & co, ili tukasake benki za kutukopesha. Mengi (au "mzawa" yoyote yule) akipata hiyo licence faida itakayopatikana ni ya kwake na ya familia yake, wewe na mimi tutafaidika nini na fact kwamba ni "mzawa mwenzetu" compared to kama angeshinda mzungu? absolutely nothing, except some theories like "atawekeza nyumbani" blah blah blah. kwa hiyo hakuna sababu ya msingi ya kutenga vitalu vya "wazawa" vitalu vyote vimilikiwe na serikali kwa niaba yetu sote.
Option bora ambayo ni fair kwa watanzania wote ni ku-auction vitalu to the highest bidder baas! Kama bid zitagongana na za wazungu, hapo nakubali tumpendelee mzawa. lakini sio kuweka baadhi ya vitalu tukadanganyana kuwa ni vya "wazawa" wakati dereva bodaboda, mwalimu, mimi, wewe na majority ya watanzania wote (over 40 mil) hatutaweza kununua hata fomu ya maombi! Na huyo Mengi atayepata atakwenda kukopea mtaji.
Na kumbuka hapa ni ku-bid ili kupata 25%, 75% tayari ni ya watanzania through TPDC, kwa hiyo wether anapata mzungu au mzawa faida kubwa ina guarantee ya kubaki Tanzania.
Kiukweli nitakubaliana na Mengi pale atakapotoa mfumo ambao kila mtanzania atakuwa na nafasi ile ile atakayokuwa nayo yeye kupata hizo leseni. Mfano wa kimasihara, labda majina yetu watanzania wooote yaingizwe kwenye bahati nasibu, atakayeshinda anapewa kitalu cha "wazawa" aende kusaka benki, hapo itakuwa fair!

3. Sidhani kama Magufuli anatoa tu kazi kwa wakandarasi wazawa hata kama hawana vigezo, ninavyojua ni kwamba kama vigezo viko sawa ndipo hoja ya uzawa inakuwa na nafasi. Hata katika hili la mafuta kama "mzawa" atafungana na wazungu katika vigezo vya msingi basi apewe sina tatizo na hilo.

4. Faida kubwa zaidi katika mambo ya mafuta ni sekta ya huduma. Nilitegemea TPSF inayoongozwa na Mengiwashinikize sera ya "makampuni ya wazawa" katika kutoa huduma kwa hayo makampuni ya uchimbaji katika mambo mbalimbali kama chakula, ulinzi, usafiri, IT, Engineering, n.k badala yake wamejikita kutaka ubilionea wa bure wa ku=flip concessions kama wanaijeria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…