Bilionea Mohamed Dewj Arudi kuifadhili Simba

Bilionea Mohamed Dewj Arudi kuifadhili Simba

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Mbunge wa Singida na Mfanyabiashara mkubwa mwenye umri mdogo mwenye mapenz kwa Simba mohamed Dewj amerud kuja kuifadhiri team yake kipenz Simba Sports Club maarufu kama Mnyama yenye maskani pale kariakoo mtaa wa Msimbazi.

Bwana Dewji ambaye pia amepost picha za jezi ambazo amewanunulia simba kwa ajili ya kuonesha namna gani amekuwa na mapenz na team hii ingawa alijiweka kando kidogo na mambo ya mpira.

jambo hili limewafurahisha wana simba wengi hasa kwa kuwa kijana huyu amekuwa akijiamini na biashara zake ni halali hivyo anafanya udhamini kwa nia njema na si kwa ajili ya kuitumia team kufanya biashara haramu kama wadhamini wengine wanavyofanya. kwenye jarida maarufu dunian la forbes dewj anatajwa kuwa ni Billionea Mdogo Africa.

Wanasimba sasa kaeni tu mkao wa kufurahia matokeo ya udhamini wake.
 
hatutaki ufadhiri wako ukiona kuna mhindi simba ndio unajifanya ufadhiri akitoka hufadhiri
 
Mnyama ni mnyama tu, vyovyote itakavyokuwa, kama kweli au la, ila nijuavyo, Mohamedi eats, sleeps and breathes Simba. Kama ni habari za kweli, itawapa na wachezaji morali sababu haya mambo ya kwenda kucheza ndondo kupata hela ya mafuta yataisha!!
Pamoja na hayo, viongozi wa simba sijui wataamka lini, Simba ina rasilimali kibao ila bado omba omba sababu ya njaa za watu!
Labda siku moja mtu mwenye pesa na sio mwanachama wa mafia atakapochukua uongozi ataipeleka Simba inapotakiwa kuwa, sio kuitumia kupiga hela!
 
hzi habari ni za kweli zimesomwa kwenye magazeti ya leo asubuh. na ningependa salamu hizi ziwafikie Bantu lady, makoye, yahoo na wengine popote walipo . ujumbe unasema "simba hata akizeeka vipi hawezi kuwa paka"
 
Last edited by a moderator:
wakimataifa punguza munkari kaka ...soka la bongo bila ufadhiri kwa sera za club zetu ni ngumu wachezaji wanateseka sana we hujui ndo maana habari hizi tusizilete na ushabiki. kama kaona kuna wahindi au waarabu its ok la msing aisaidie simba wachezaji hawana pesa z utosheleza. na haya mambo ya ufadhiri ni makubaliano mbona mwenyekiti wa simba ni mwafrika pure wa mbeya?makamu n.k so tuache ukaburu.
 
Last edited by a moderator:
Hivi yule mhindi mdhamini wa wavuvi wa kambale pale karibia na Fire anashika nafasi ya ngapi vile, maana sidhani kama anafahamika hata nje ya mipaka ya Dar es salaam.
 
Mpira km spots zingine ni gharama sana chukua ulaya na tp mazembe
 
hzi habari ni za kweli zimesomwa kwenye magazeti ya leo asubuh. na ningependa salamu hizi ziwafikie Bantu lady, makoye, yahoo na wengine popote walipo . ujumbe unasema "simba hata akizeeka vipi hawezi kuwa paka"
Simba hata asipozeeka ni jamii ya paka
 
Last edited by a moderator:
Hakuna mfanyabiashara yeyote mkubwa aliye serious atakayefanya ujinga wa kujihusisha na Simba au Yanga.

I personally know Mo. He's a corporate animal ambaye anataka kujenga dynasty kwenye nyanja ya biashara ya kimataifa. He's smart enough to know kwamba Uyanga na Usimba ni serious distraction and a potential damage kwa reputation ya jina lake kubwa analoendelea kulijenga kimataifa.

So, mleta habari usilete taarifa za kutunga hapa JF.
 
Alikuja bilionea malkia wa nyuki akakawakimbiae,sasa anakuja balkia wa nyuki,milionea naye atase...bila mafanikio yoyote
 
hzi habari ni za kweli zimesomwa kwenye magazeti ya leo asubuh. na ningependa salamu hizi ziwafikie Bantu lady, makoye, yahoo na wengine popote walipo . ujumbe unasema "simba hata akizeeka vipi hawezi kuwa paka"
Kweli wabongo ni shida yaani badala ya kuhangaika kutafuta vitega uchumi vyenu, ili timu iwe na vyanzo endelevu vya mapato, bado mnaona sifa za kutegemea pesa za mtu mfukoni!!! na ndio zimewafikisha hapo, timu gani zina miaka 80 toka zianzishwe hata uwanja wa mazoezi tu hamna!!! Na wao wameshaona kuwa hizi timu ni machaka ya wajinga ngoja tupige tu, bora hata kidogo udhamini kuliko ufadhiri. Mkiambiwa hizo timu ziwe makampuni hamtaki, kadi ya uanachama tu kulipia shida, ila unataka kwenye maamuzi uhusishwe hiyo ya wapi??? Matumizi ya timu kwa mwezi karibu 80M,mapato hayajulikani, eti wadau wanatoa pesa zao mifukoni!! Kuendesha mpira kiujanja ujanja ni ngumu, bora hata huyo Mo dewji mngesema mnamuuzia timu, ijulikane moja tu, kwenye kununua wachezaji hamtoi hata senti ila akiuzwa utasikia pesa alizouzwa fulani ziko wapi!??? mbona wakati ananunuliwa hamkuhoji pesa zimetoka wapi?!! Ila kwakuwa mashabiki wa hizo timu ndio wale wale acha wajanja wakamue, Uwanja wa bunju uko wapi? 2B, zinatakiwa kujenga uwanja huo, na watu juzi waanaambiwa match za simba za pre season za mwakani zinachezewa hapo!!! wajinga makofiii, Leo anaibuka shabiki wa hizo timu zenu kongwe ana beza eti uwanja wa azamu uwanja gani wenye kuchukua watu 7000!!!wakwako wa watu hata 20 uko wapi?? Kazi kuendekeza uchawi tu, na hata siku hizi ushabiki wa mechi zenu umepungua sana, kwani watu wahaongei ki taalam ni kishabiki zaidi!! eti hata timu yangu iwe mbovu aje bora nitafungwa na stand utd lakini sio wewe!!! kisa amepitia huko anakojua yeye na kupata hayo matumaini, timu gani ukifungwa tu ndio kocha kwa heli, kwani ligi nzima ni kumfunga yanga au simba tu!?? Ningekuwa na uwezo bora haya ma timu mawili yangefutwa tu. ohoo mala hizo milioni 100,za haki za kuonyeshwa kwenye tv ni ndogo, za kwako nyingi ziko wapi?!!! tena mzee AKilimali nasikia cku hizi anajiita ABROMOVIC!!!!
 
Last edited by a moderator:
Alikuja bilionea malkia wa nyuki akakawakimbiae,sasa anakuja balkia wa nyuki,milionea naye atase...bila mafanikio yoyote

Avatar yako naituma yahoo wakuchukulie hatua inaogopesha watu.
 
Wote mnaoshabikia ufadhili wa hao watu mnashangaza.Kwani moo ni Mara ya kwanza kufanya hivyo!.Ni kipi kipya anakuja nacho?.Akiwa mfadhili kuna siku Simba itafanana na TP Mazembe?.Au anafadhili ili mambo ya kukwepa kodi kupitia vilabu kama walivyowahi kufanya wengine yaendelee?.
 
udhamini na ufadhili ni mzuri lakini tatizo ni mfumo Wa uendeshaji Wa timu
 
Alikuwepo sana siku za nyuma la kujiuliza kitu gani kilimwondoa. Je sababu haipo tena? Anaweza kusaidia kama mwanachama/mshabiki lakini la kurudi kudhamini tena, I doubt! Si ndiyo huyo alinunua timu vikamshinda?
 
Huyu MO ile timu yake ya Mto Singida hivi iko wapi wadau?
Au washashiba ndo kahamia simba?
 
waswahili bwana mi huwa wananishangaza sana. MANJI ALIWEPO YANGA it is ok. ila MO DEWJ akija SIMBA inaonekana tumepotoka... hii ni double standard. mpira wa Team za SImba na YAnga kufika hatua ile mnayoitaka ni gumu na wengi wenye akili wanalijua hili ....ilikuwepo yanga kampuni na yanga asili what happened? ninyi mnaongea hapa weng hamjui historia za timu hizi na ndo maana unavyoiona azam hata ingechukua kombe la dunia bado haiwezi kuja kuifikia simba au yanga hapa nchini kwa wapenzi na ushindan . haya mambo yana mizizi msidhani tu inawezekana siku moja ikatokea simba ikawa kampuni au yanga ... wafadhiri wana faida na hasara zake. tusisahau hawa ni wafanyabiashara nao wanataka faida ktk mambo yao hala hala tu isiwe ya kupitisha madawa ya kulevya kama anavyofanya yule mhindi mwingne wa upande ule. kujidai unashabikia man,chelsea ukaponda simba na yanga huu ni umaamuma mwingne wa aina yake.... ni upumbavu tu... ashakum si matusi. hizi team watu mmeanza kuzifahami miaka ya 90 hapa wengine mlikuwa wadogo mpka miaka ya 2000s leo unajidai kuziponda hizi team wakati ndo msingi wa ushabiki wa mpira nchini, huu ni ulimbukeni tu na wengne kwa kupofushwa macho wanapinga kila la simba na yanga..... sana sana unaonesha tu kuwa huujui mpira .... unajidai mi bora nishabikie arsenal kana kwamba nazo hazina mizengwe hazipotezi mechi ...mmesahau man united ilikuwa inashika nafasi ya ngap? acheni huo ubohora.
 
Back
Top Bottom