Bilioni 11 zawekezwa NSSF na Benki ya Maendeleo (TDB) kuhamasisha ukuaji wa sekta ya biashara katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki

Bilioni 11 zawekezwa NSSF na Benki ya Maendeleo (TDB) kuhamasisha ukuaji wa sekta ya biashara katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Takribani shilingi bilioni 11 zimewekezwa katika Shirika la Taifa (NSSF)kuhamasisha ukuwaji wa sekta ya biashara katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki na Benki ya Maendeleo (TDB).

Uwekezaji huo unalenga kupanua wigo wa benki na kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wanachama wake ambao utawawezesha kununua hisa 800, sawa na asilimia 0.64.

Kiasi hicho cha hisa, kitaupa mfuko huo wa hifadhi ya jamii uhakika wa mgao wa asilimia 25 kila mwaka.

“Uwekezaji huo unaifanya benki kuwa na mtaji mkubwa katika nchi wanachama. NSSF pia itaongeza mapato yake na uwezo wa kuhudumia mafao ya wanachama kwa wakati,” alisema Mkurugenzi wa hifadhi ya jamii, Festo Fute,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam Ijumaa hii wakati wa hafla ya kukabidhi hati ya hisa, ambapo aliupongeza mfuko huo kwa uamuzi wake utakaowezesha kunufaika na wadau ambao pia ni wanachama wa benki hiyo katika nchi 20.

Amesema ununuzi wa hisa 800 ni uwekezaji mkubwa wa mtaji uliowezesha bodi ya benki hiyo kutoa gawio la asilimia 25 kila mwaka ambapo mapato hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kulipa mafao kwa wakati kwa wanufaika wa mfuko huo.

Aliongeza kuwa hiyo ni fursa kwa mifuko mingine ya usalama kuangalia uwezo wao wa uwekezaji na kutumia fursa hiyo kwa vile walihamasishwa na serikali kuwekeza katika uwekezaji wenye faida.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema Tanzania imewekeza TDB kwa asilimia 6.03 ya hisa, na kushika nafasi ya ‘grade A,’ na kubainisha kuwa mfuko huo umefadhili miradi minane ya maendeleo yenye thamani ya Dola 580 milioni (takriban Sh1.3 trilioni).

“Uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza mapato yetu kupitia gawio la mwaka na ongezeko la thamani ya hisa. Naishukuru serikali kwa kufungua zaidi mipaka na kuturuhusu kuwekeza katika nchi wanachama wa kikanda,” amesema.

Alisisitiza kuwa uwekezaji huo utaongeza wigo wa fursa na uamuzi uliopo katika kanda, pia itakuza ustahimilivu wa fedha na kuongeza ukwasi pamoja na ulipaji wa mafao ya wanachama kwa wakati.

Naye , Rais wa TDB na Ofisa Mtendaji Mkuu, Admassu Tadesse amesema "NSSF ya Tanzania imekuwa taasisi mpya ya pili kuwekeza na benki hiyo, ikijiunga na jumuiya ya wanahisa, zaidi ya uwekezaji mwingine wa mtaji kutoka kwa wanahisa waliopo."

Sambamba na wanahisa wakubwa kama vile Tanzania, kuendelea kujiamini kwa wawekezaji wa kitaasisi katika uwezo wa kutekeleza majukumu yao ni chachu kubwa ya juhudi za pamoja za kuleta maendeleo endelevu katika kanda nzima, alisema.

IMG-20221018-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom