Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita amefika Shule ya Sekondari Ndedo na kukabidhi Kompyuta Tano (05), Printa (Printer), Projekta (Projector) na Mashine ya Photocopy mpya kwaajili ya kufundishia na kuwataka Wanafunzi kusoma kwa bidii kujiongezea Maarifa.
Mhe. Edward Ole Lekaita ameungana na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Mollel kushiriki uzinduzi wa Albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili, Paulo Siria uliofanyika katika uwanja wa michezo Kibaya.
Mhe. Edward Ole Lekaita ameambatana na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Mollel kukagua mradi wa Kituo cha Afya Mwanya ambapo amewataka Wananchi wa Njoro kuendelea kuiamini Serikali ya Awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Vilevile, Mbunge Edward Ole Lekaita na Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Mollel wamekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa majengo Matatu (03) ya Hospitali ya Wilaya ya Kiteto iliyopo Kibaya. Mhe. Dkt. Mollel amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za miradi ya Afya.
Mhe. Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Uwekezaji wa Shilingi Bilioni 3.5 ambapo Shilingi Bilioni 2.6 ni kwaajili ya Huduma za Afya na Shilingi 900,000,000 ni kwaajili ya Majengo Matatu Hospitali ya Wilaya, Vituo Viwili vya Afya na Vifaa Tiba.