Kuibiwa mabilioni siyo sasa imekuwa ni kawaida tu kati ya mambo wanayofanyiwa Watanzania? Hakuna kitu chochote kitakachotokea kwani walioiba watalindwa ile mbaya.
Ukiacha wananchi wachache sana, wengi ni kama "sheep in the field" (kunradhi kwa maneno haya kwani ni onyesho langu la huzuni kubwa). Hawatafanya chochote kwani wengi wao hata magazeti yanayoandika haya yote hawasomi, sana sana hununua na/au husoma magazeti ya udaku tu na yale ya michezo ambayo yote hayo yanasheheni asilimia 90 uongo. Saa ngapi wafikirie wafanye nini wanapoibiwa mchana mchana?