Hata Dr Slaa akifia majukwaani kwa kuwaeleza wananchi wizi huo wa CCM wqananchi wengin hawatomuelewa kabisa. Wengi kwanza hawajui TANAPA ni nini.
CCM inajua inachokifanya kwa kutambua kuwa nchi hii is blessed with teeming herds of sheep instead of humans!
Wewe una jukumu la kumsaidia Slaa kumuelimisha baba yako na mama yako na bibi na babu yako na mzee jirani yako kule kijijini, shangazi mjomba etc. Probelm yetu hapa tunafungua midomo tu, lakini hatufanyi kivitendo, si ajabu ni wachache wetu tumejiandikisha kupiga kura.
Kama wachangga wanavyofunga safari wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka kwenda makwao, vivyo hivyo tunapaswa sote kufunga safari kwenda vijijini mwetu wakati huu wa kampeni kwenda kuwajuza na kuwahubiria wazee wetu na kuwaonya kuwa hali yao itakuwa mbaya kwa sababu hali yetu huku mjini pia itakuwa mbaya na kile chochote kitu tunachowatumia kitapungua kama hawatatumia kura yao vizuri kuondoa ukiritimba na udhalimu wa ccm. I tell you CCM ikiingia madarakani tena watanzania watarajie hali ngumu mno ya maisha, mara nyingi raisi hafanyi mengi kwenye kipindi chake cha pili, zaidi ya kuiba, mtakumbuka Mkapa aliharibika katika kipindi chake cha pili, but more precisely baada ya Mwalimu kufariki
Kuna fedha nyingi zilipelekwa NHC kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu (Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa NHC alipohojiwa na Mwakai wa Kuhenga). Nawaasa Chadema waangalie vizuri NHC kwa kuwa ni possible ikawa mojawapo ya conduit ya kufuja fedha za Watanzania. Japo mkurugenzi wake ni mtu makini lakini anaweza kubanwa na machinery za CCM akapotea stepu. This time hawatachota BOT, but watachota kusikojulikana kama Tanesco, NHC etc.
Sh 50BN hazitatosha kwa kampeni za JK na CCM yake. Kama mwaka 2005 walichota 133bn za EPA this time is even more. Na kumbuka mwaka 2005 JK alikuwa anapendwa kwani wengi walikuwa hawajamshitukia kuwa ni feki, this time around things are different na pia ujio wa Dr Slaa, unafanya kibarua chake kiwe kigumu. JK kipindi chake cha kwanza ameshuhudia wapinzani wakiimarika kutokana na utendaji mbovu wa serekali yake ni ufisadi, kitu kianchofanya awamu yake ya pili kuwa ngumu kuitetea.
So CCM watahitaji fedha nyingi zaidi ya 50bn, hapo ndipo penye kirumbe rumbe, yetu macho, Chadema, tupieni jicho mashirika ya umma, mihela itachotwa huko vibaya sana!!