Katika kipindi cha Uongozi wa Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuanzia Machi, 2021 hadi Machi 2025, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepeleka zaidi Shilingi Bilioni 86 Manispaa ya Lindi kwa ajili ya utekelezaji wa Miundombinu mbalimbali ya Elimu, Afya, Maji, Barabara, Utawala, Viwanda na Biashara, Ujenzi na Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva alisema kuwa miongoni mwa mradi mkubwa ambao umepata fedha nyingi ni shule ya wasichana Lindi iliyojikita katika mchepuo wa masomo ya sayansi, imepata zaidi ya Bilioni 4 hadi kukamilika kwake.