Baada ya Rapa na mfanyabiashara, Billnass kumzawadia mke wake, Nandy, gari la kifahari siku ya kuzaliwa kwake, sasa ni zamu ya mtoto wao kupata zawadi ya gari. Kupitia mtandao wa Snapchat, Billnass alionesha zawadi ya gari aina ya Alphard aliyomzawadia mtoto wake baada ya kufikia kuhitimu masomo.
Billnass aliahidi kuwa akifika darasa la kwanza, atamzawadia mtoto wake gari aina ya Escalade. Aliandika kwenye mtandao wake: "Zawadi ya Naya ya graduation kwenda KG One, Nandy mpaka akifika la kwanza, ni Escalade tu."