Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bima gani kwa maana ya Kampuni au aina ya Bima??Nataka ninunue bajaj kwa ajili ya biashara je bima gan ni nzuri
Natanguliza shukran zangu za dhati
Thanks !! Nimekusoma nimepewa copy ya mkataba apa kuna kifungu kimeandikwa io comprehesive insurance au bima kubwa nimeelewa kiasi naomba unipe ufafanuzi kidogo comprehesive bima ni nn ? Na je kuna aina gan zengine za bima ?Bima gani kwa maana ya Kampuni au aina ya Bima??
Kama ni Kampuni zote zinafanana tu, zaidi ningekushauri Alliance Insurance ninayoitumia.
Kama ni aina ya Bima basi Bima Kubwa (Comprehensive) ingefaa zaidi ili ikulinde na Chombo chako wewe.
Aina za Bima ziko nyingi, Ila kwa swala lako niseme ziko mbili tu, Bima ndogo na Bima kubwa. Kizungu ndio hiyo"Third party" na "Comprehensive".Thanks !! Nimekusoma nimepewa copy ya mkataba apa kuna kifungu kimeandikwa io comprehesive insurance au bima kubwa nimeelewa kiasi naomba unipe ufafanuzi kidogo comprehesive bima ni nn ? Na je kuna aina gan zengine za bima ?
Kuhusu swala la kampuni its clear nimekuelewa
Nimekusoma ebu naomba unisaidie gharama za comprehesaive bimaAina za Bima ziko nyingi, Ila kwa swala lako niseme ziko mbili tu, Bima ndogo na Bima kubwa. Kizungu ndio hiyo"Third party" na "Comprehensive".
Third party/Bima Ndogo faida yake ni kua bei/gharama yake ni rahisi tu. Hasara yake ni kwamba ikitokea jambo lolote baya (kuibiwa/ajali/kuungua) kuhusu chombo chako, yenyewe itamfidia "Kitu/Mtu" wa tatu tu. Wewe dereva na Chombo chako hamtahusika katika kufidiwa huko.
Comprehensive/Bima kubwa hii ni kua ikitokea jambo lolote baya (kuibiwa/ajali/kuungua) kuhusu chombo chako yenyewe itamfidia kila alieathirika na ajali hiyo ukiwemo wewe dereva pia. Na chombo chako kama kimepata madhara nacho kitafidiwa pia.
"Kitu/Mtu" wa tatu ni Nani? Hapa wewe unaendesha hicho chombo/Bajaji Ni wa Kwanza. Chombo/Bajaji yako ni ya pili, utakae msababishia ajali iwe ni mtembea kwa miguu, au chombo cha moto au hata nyumba, kibanda umegonga ndio "Kitu/Mtu" wa tatu.
Ndugu wewe ni mtaaluma wa bina?unatoa ufafanuzi mzuri hongera sanaGharam ni laki tano kwa mwaka