Bima ya Afya - Inakuwaje Mstaafu wa Serikali anufaike na Mstaafu wa sekta binafsi asinufaike?

Bima ya Afya - Inakuwaje Mstaafu wa Serikali anufaike na Mstaafu wa sekta binafsi asinufaike?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nasikiliza hapa mkurugenzi wa Bima ya Afya NHIF (Benard); Kaulizwa hivi, Mtu akistaafu inakuwaje?

Kajibu kuwa kwa Mtumishi wa Uma ataendelea kupatiwa huduma. Mtangazaji hakuwa makini kumuuliza na kwa mtumishi wa Secta Binafsi inakuwaje? shame!

Yaani kwa mfano; Raia mmoja aajiriwe Serikalini afanye kazi miaka 20 na mwingine aajiriwe Shirika Binafsi afanye kazi miaka 20 wote wakiwa wanachama wa Bima ya TAIFA
ILA wakistaafu Aliyekuwa Serikalini anatambulika na aliyeko Shirika Binafsi hatambuliki?

Sijui kama watunga Sheria wetu wanafaham hili!
 
Kwani Mkurugenzi alikua anatoa majibu ya wa Sekta ya Umma ama binafsi ama wote?

Tuanzie kwenye swali lenyewe
 
Back
Top Bottom