Bima ya afya itumiwe hadi kwa waganga wa kienyeji

Kichochoro

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2017
Posts
1,135
Reaction score
1,167
Naandika kama ushaur kwa serikali ya Tanzania hasa wizara ya afya hasa upande bima za afya yaani National health insurance fund (NHIF) zimeonekana kusaidia sana hasa kwa watu wanapougua na kutibiwa kwa kutumia bima hzo.

Ushaur wangu kwa wizara ya afya kama inawatambua wanganga wa kienyeti hasa wenye leseni nazinatambulika kwa level kuanzia ngazi ya wilaya,mkoa hata taifa waganga nashaur washauriwe/waombwe pindi mtu anapougua na huenda ugonjwa wake ukaonekana unaweza kutibika kienyeji bas.wagonjwa hao watumie bima za afya kama ilivyo kwenye mahosptal yetu ili watu waweze kwenda kutibiwa hata kwa hao waganga wakienyeji bila kuogopa garama za matibabu.

Baadhi ya watu wenye bima hzo wametibiwa kwa waganga hao na wengne wanashindwa kwenda kutibiwa kulingana na garama zakugarimia matibabu.

Hvyo naishaur serikali hasa kupitia wizara ya afya kutengeneza mfumo ambao utakuwa wezeshe watu wenye bima watibiwe popote as they wish!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matunda, monga za majani ni zaidi ya sindano..

Mwili nao ni nani unataka nyama tu.
 
kwanza visajiliwe hivyo vilinge vyao ili watambuliwe ,na wasiwe waganga wanaopiga ramli chonganishi ,na wasiwe wanaotumia viungo vya binadamu.
Dawa zao ni lazima ziainishwe ili zijulikane majina yake na viwango vyake kitaalamu.Kwa hili italazimu idara nyingine kama za viwango na bodi ya madawa ishiriki kutoa idhini ya dawa hizo kutumika kwa ubora na usalama wa afya za watumiaji ziwe salama.
Serikali itowe vigezo kwa wale wenye mapepo watapungwa kwa bei gani kwa mujibu wa ukubwa wa tatizo la pepo huyo.
Iwe marufuku waganga kutumia damu kama dawa,au Limbwata za kina mama dhidi ya waume zao nazo pia ziwekewe viwango vya bei,
 
Nadhani hapa ulikuwa unazungumzia wale watu wa dawa za asili, herbal clinics tu. ama na wale wa vilinge vya ramli pia???
 
Asante kwa kuongeza mwana jf
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…