Msumbeni2015
New Member
- Jul 22, 2021
- 2
- 1
Kwa kuwa Serikali ina mpango wa kutoa bima ya afya kwa kila Mtanzania nimepata wazo la namna bima hyo inavyoweza kufanyika kwa kutumia TOZO ZA MUDA WA MAONGEZI,kwa kuwa idadi kubwa ya watanzania wanamiliki LAINI za simu hivyo nashauri yafuatayo:
1. Serikali iweke tozo mpya katika muda wa MAONGEZI ambapo raia akiweka vocha kwa ajili ya muda wa MAONGEZI akatwe kiwango fulani amabacho ni HIMILIVU na kitumwe katika MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA Kwa majina yaleyale yalio sajiliwa katika laini husika Kama MCHANGO wa mwanachama na michango hiyo ikifikia kiwango cha chini cha Tsh 20,000/= basi raia au mwanachama huyo aweze kupatiwa kadi yake ya bima ya afya kwa ajili ya kupata huduma za afya BURE (Utaratibu wa Bima) katika vituo vya afya au hospitali yoyote nchini.
WATEGEMEZI
Kwa kuwa UMILIKI na USAJILI wa laini za simu ni kwa waliofikisha umri wa miaka18 ni wazi WATEGEMEZI katika bima hii watakuwa watoto ambapo nashauri mwanachama au raia mmoja ambae Makato yake yamefika Tsh20,000/=Kama MICHANGO yake ya bima ya afya basi aruhusiwe kuwa na WATEGEMEZI watoto wawili (sio lazima watoto wa kuwazaa) kwahyo Kama mchangiaji ni MUME na amefikisha Makato stahiki atakuwa na WATEGEMEZI watoto wawili na Kama mwanachama au raia ni MKE na amesajili laini yake kwa majina yake na atakuwa amefikisha Makato stahiki basi na yeye atakuwa na WATEGEMEZI wawili hivyo hii itapelekea mke na mume kuwa na WATEGEMEZI watoto wanne(sio lazima wawe watoto wa kuwazaa)
RAIA
Raia watakuwa na wajibu wakutembelea katika ofisi yoyote ya MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA wakiwa na vitambulisho vya uraia au namba za utambulisho wa raia ili kujionea Makato yao wanayo katwa katika muda wa MAONGEZI Kama MICHANGO yao ya bima zao za afya na Kama Makato hayo yamefika Tsh20,000/= wapewe KADI ZAO ZA BIMA kwa ajili ya MATUMIZI.
KAMPUNI ZA SIMU
KAMPUNI za simu zitakuwa na jukuma la kukusanya Makato yote na kuyatuma katika MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KWA kutumia majina yaleyele yalio sajiliwa katika laini husika inayo katwa tozo ya muda wa MAONGEZI.
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya utakuwa na jukumu la kutoa kadi za Bima ya afya mapema kwa wanachama au Raia wote ambao watakuwa wamefikisha Makato ya Tsh20,000/=ili waanze kupata huduma za afya BURE (utaratibu wa Bima)
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA)
kwa kuwa Bima hii ya afya kwa kila mtanzania inategemea UMILIKI wa LAINI za simu na UMILIKI wa LAINI za simu unahitaji uwe na kitambulisho cha uraia au namba za utambulisho wa Raia ni wazi Mamlaka ya vitambulisho vya TAIFA itakuwa na jukumu la kuendelea kutoa vitambulisho vya uraia au namba za utambulisho wa raia ili watanzania wengi wapate Bima ya Afya kwa wakati.
RAIA WENYE BIMA NYINGINE
Kwa Raia ambao watakuwa na Bima nyingine Tayari basi Bima hii ya afya kwa kila mtanzania itampa nafasi ya kuorodhesha watoto watatu ambao hawajakatiwa bima(sio lazima watoto wa kuwazaa ili wahudumiwe na Bima hii ya afya kwa kila mtanzania.
MWISHO
Kwa kuwa idadi kubwa ya watanzania wanamiliki laini za simu na kwa watoto wasio miliki laini za simu watapata fursa ya kuwa WATEGEMEZI kutoka kwa wazazi au walezi wao (watoto sio lazima wa kuwazaa) basi naamini Kama WAZO hili likiwekewa MIKAKATI THABITI litakuwa MWAROBAINI wa mpango wa kuwa na BIMA YA AFYA KWA KILA MTANZANIA.

Upvote
2